fbpx

Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Clickfarms ni neno jipya katika ulimwengu wa sasa wa kidigitali. Neno hili huwakilisha watu waliounganisha mifumo ya simu nyingi pamoja na kompyuta na kuwezesha akaunti mbalimbali feki kulike, kucomment na ata kushare mambo mtandaoni.

Tunajua kuwa mara kwa mara kampuni/taasisi huingia gharama kusafisha ‘likes’ zisizohitajika, emoji, ratings, maoni ya kipuuzi na kwa nia ya kujijengea jina mitandaoni na mwishowe kushawishi kupata matangazo yatakayoingiza fedha nyingi.

Sasa uvamizi wa hivi karibuni nchini Thailand umetoa muonekano mwingine kuhusu undani wa tasnia ya ‘Bot’, yaani ile ya ulipaji fedha kugharimia kupata likes, comments au shares zisizorasmi mitandaoni zinazotengenezwa na akaunti zinazoendeshwa na kompyuta (yaani Bots).

INAYOHUSIANA  Matangazo Ya Samsung Kuwa Vifaa Vya Kuchajia Galaxy S10!

Kwa mujibu wa gazeti la Bangkok Post, polisi na wanajeshi wa Thailand walivamia nyumba ya kupanga jirani na mpaka wa Cambodia, wakifichua kundi la wahalifu wa kimtandao (clickfarm) linaloendeshwa na raia watatu wa Kichina.

Wang Dong, Niu Bang, na Ni Wenjin wanadaiwa kuwa na shubaka za chuma ndani ya nyumba hiyo zikiwa na mamia ya simu za iPhone 4S, 5C, na 5S zilizounganishwa kwenye vioo vingi vya kompyuta.

udukuzi clickfarms

Clickfarms: Kwa ujumla, iPhone zinazofikia idadi ya 474, jumla ya kadi za simu zisizotumiwa 347,200 ambazo ni za waendeshaji wa kampuni za simu za Thailand, kompyuta 10 za mezani na vipsktslishi (laptop).

Awali, maofisa wa polisi walidhani kuwa wahalifu hao walikuwa wakiendesha kituo haramu cha kutoa huduma za simu, lakini ilibainika baadae kuwa watuhuniwa walikuwa wakifanya matukio makubwa zaidi kwa kuwa na akaunti za ‘bot’ kupitia WeChat, ambao ni mtandao wa kijamii mkubwa kuliko yote nchini Uchina.

Watuhumiwa hao watatu walisema kuna kampuni ya Uchina (ambayo walikataa kuitaja jina) iliwapatia simu na huwalipa $4,403 (takribani Tsh. Milioni 10) kila mwezi ili kufanikisha mauzo ya bidhaa zake zinazouzwa nchini Uchina kupitia mtandao wa WeChat kupitia Likes nyingi, na comment zinazosifia bidhaa.

Makao makuu ya mtandao huo wa kihalifu yamewekwa Thailand kutokana na ukweli kuwa gharama za matumizi ya simu nchini humo ni za chini zaidi kulinganisha na maeneo mengine mengi.

Hivi sasa polisi wa Thailand wanachunguza ni kwa namna gani watuhumiwa hao walifanikisha uingizaji  kimagendo wa simu hizo nyingi nchini humo.

Pili, wahalifu waliwezaje kupata kiasi kikubwa cha kadi za simu za kampuni mbalimbali nchini humo ambazo kisheria hutakiwa rekodi zake ziwe katika kumbukumbu ya  taarifa za wateja mara tu zinapounganishwa hewani na kuanza kutumika.

Makala hii imesasishwa(updated) – 2.08.2018

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.