Mechi za La Liga kuonyeshwa bure na Facebook

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Facebook inategemea kujizolea watumiaji wengi wa mtandao huo wa kijamii maarufu zaidi duniani kwa hatua yake ya kuonyesha mechi za La Liga bure kabisa kwa misimu mitatu mfululizo.

Hatua hiyo inakuja kama kuongeza ushindani kwani Amazon nao wana kibali cha kuonyesha mechi za ligi kuu ya Uingereza. Facebook watakuwa wakionyesha mechi hizo za ligi kuu ya Uhispania kuanzia msimu ujao wa ligi hiyo.

Mpango huo wa Facebook hautawafaidisha watu wote duniani ila ni kwa baadhi ya nchi tu ambazo ni Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, India, Nepal, Maldives, Sri Lanka na Pakistan.

Mechi za La Liga

Kabla ya mechi utakuwepo uchambuzi wa soka kutoka kwa Joe Morrison, Michel Salgado na Garcia offering kisha mechi kuonyeshwa mubashara.

Hii inamaanisha Facebook itakuwa ikionyesha jumla ya mechi 380 kwa watumiaji wa Facebook takribani mil. 348 kutoka kwenye nchi hizo zilizopo Kusini mwa bara la Asia huku India pekee ikikisiwa kuwa na 270m (watu wenye akaunti Facebook).

Haijawekwa wazi ni kiasi gani cha pesa Facebook wamelipa kuweza kupata kibali ya kuonyesha mechi hizo mubashara kwa muda wa misimu mitatu ijayo lakini inaaminika kuwa ni kiwango kikubwa.

Vyanzo: The Guardian, CNBC, Sport English

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Tecno waingia mkataba wa kimatangazo na timu ya Manchester City
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.