fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Tanzania Teknolojia

Mtandao wa Smile Kusambaa Zaidi Nchini: Kuja na Huduma za Kupiga Simu

Mtandao wa Smile Kusambaa Zaidi Nchini: Kuja na Huduma za Kupiga Simu

Spread the love

Mtandao wa Smile Tanzania ambao ni moja kati ya mtandao mkubwa kabisa unaotoa huduma ya intanet katika mfumo wa 4G umejipanga vyema kuanza kusambaza huduma yao katika maeneo mengi zaidi.
Wakiwa na takribani bajeti ya zaidi ya dola milioni 365 za kimarekani wanategemea kusambaza huduma zao katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Dodoma, Moshi, na Morogoro.

Mpango wao unajumlisha mpango wa kuwa na uwezo wa kutoa hadi huduma za maongezi ya simu kama ilivyo kwa mitandao mengine kabla ya mwisho wa mwaka 2016. Hayo yalisemwa na meneja mkuu wa Smile nchini Tanzania, Bwana  Eric Behner, wikiendi iliyopita katika shunguli waliyoiandaa kutambulisha rasmi mipango yao ya ukuaji.

SOMA PIA  Mambo/Maboresho ambayo Apple wanayafanyia kazi

Kwa sasa mtandao wa Smile unatoa huduma zake za intaneti ya kasi ya 4G katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha tuu. Na ata kwa Dar es Salaam kuna maeneo mengi pembezoni mwa mji huduma yao inakosekana.

Hivi karibuni wametambulisha vifurushi vidogo zaidi.

Hivi karibuni wametambulisha vifurushi vidogo zaidi.

Kwa kiasi kikubwa ni jambo zuri wao kuzidi kukua na kuweza kuzidi kuleta ushindani katika utoaji huduma ya intaneti ya kasi zaidi nchini. Suala la bei za bando zake bado ni tatizo kidogo lakini ni vizuri kwao kuamua kuleta bando mpya za bei rahisi zaidi, bando wanazoziita Smile Lite.

SOMA PIA  Uwezo wa kutuma ujumbe wakati mwingine kwenye Gmail

Je wewe unamaoni gani juu ya hili? Ushawahi kutumia intaneti ya mtandao wa Smile? Tuambie kuhusu kasi yake.

Soma Pia: Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G n.k

Vyanzo: IPPMedia na vyanzo vingine mtandaoni

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] unakumbuka Septemba mwaka jana tuliandika kuhusu mafanikio yao ya kupata takribani dola milioni 365 kwa ajili ya kuzidi kuwekeza ka… hii ikiwa ni pamoja na kusambaza huduma hiyo kwenda sehemu […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania