fbpx
Google, Teknolojia

Google warahisisha upatikanaji wa taarifa za COVID-19

google-warahisisha-upatikanaji-wa-taarifa-za-covid-19
Sambaza

Hivi sasa hakuna chaneli kwenye runinga/redio, tovuti, n.k usisikie habari kuhusu virusi vya Corona ambavyo kimsingi vinasababisha homa kali ya mapafu. Kutokana kwamba hivi sasa ndio ugonjwa ambao umeshachukua maisha ya watu duniani kote Google wamerahisisha upatikanaji wa taarifa za COVID-19.

VIrusi vya COVID-19 ambavyo viliikumba Uchina mwezi Desemba 2019 na baadae kuenea mataifa mengi duniani na kuchukua maisha ya wazee kwa asilimia kubwa na mpaka leo bado wagonjwa wapya wanaendelea kugundulika, wengine wanapona lakini bila kusahau vifo; Marekani inaogoza kwa kuwa na watu wengi zaidi waliokufa kutokana na virusi hivyo.

Sasa Google wameamua kutenga kipande kidogo ambacho ukiandika “COVID-19” utaweza kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na ugonjwa huo ikiwemo utangulizi kuhusu virusi hivyo, dalili zake, namna ya kujikinga, matibabu yake lakini vilevile takwimu za nchi mbalimbali ambazo tayari wagonjwa wamegundulika na kuingia kwenye rekodi za watu wanaougua, waliopona, n.k.

taarifa za COVID-19
Taarifa mbalimbali zinazohusu virusi vya Corona zinapatikana kwa urahisi sana kwenye Google.

Virusi hivi vimesababisha shughuli nyingi duniani kusimama kwa muda jambo ambalo linayumbumbisha uchumi wa ulimwengu na hivi karibuni Google na Apple walikubaliana kushirikiana kutumia teknolojia kuondokana na shida hiyo iliyoikumba sayari yetu.

Angaalizo! hatua hii ya Google kusogeza karibu taarifa zinazohusu virusi vya Corona zisitufanye tukapuuza maelekezo tuyayopewa na mamlaka husika kwenye nchi zetu.

Vyanzo: The Verge, Google

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Tafuta Mtu Yeyote Mwenye Simu kwa Njia Hizi
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|