Betri za simu zetu zimekuwa kiungo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa unaweza kufanya mawasiliano kwa muda mrefu/mchache kulingana na matumizi ya simu janja yako kwa muda wote mpaka pale utakapohitaji kuichaji tena.
Katika toleo jipya la iOS 11 lililokuja moja kwa moja kwenye matoleo ya simu janja mpya kutoka Apple bila kusahau kwa wale waliofanya masasisho ya programu endeshaji (upgrading) kutoka toleo la zamani na kwenda kwenye toleo la iOS 11. Yamekuwepo malalamiko ya hivi karibuni tangu toleo hilo jipya lianze kupatikana kuwa linamaliza chaji ya simu janja (iPhone) kwa haraka sana.
Kwa utafiti uliofanyika kwa watumiaji wa iPhone na iPad imebaniki kuwa kwa toleo la iOS 10 vifaa hivyo vilidumu na chaji kwa wastani wa dakika 240 kulinganisha na toleo la hivi sasa la iOS 11 ambapo vifaa hivyo vinadumu na chaji kwa wastani wa dakika 96 tu 🙄 🙄 🙄
Nini ufanye ili kifaa chako kinachotumia iOS 11 kikae na chaji kwa muda mrefu?
Suala zima la kufanya simu yako ikae na chaji kwa muda mrefu ni jambo la kuzingatia sana na uzuri ni kwamba kufanikisha hili huitaji kuwa na uwezo sana kuweza kufanikisha bali ni kufuata maelekezo yafuatayo ambayo ni rahisi sana kuelewa:-
>Zuia programu tumishi kufanya kazi hata kama hazitumiki kwa muda huo (background apps). Moja kati ya vitu vinavyomaliza sana chaji kwenye simu ni background apps ambazo hata kama hutumii app fulani ilimradi tu umeruhusu intaneti ifanye kazi basi programu tumishi hizo zenyewe zinaendelea kutumika na kupelekea kifurushi chako cha intaneti kisha bila hata ya wewe kutumia sana intaneti. Kuzuia unaingia Settings > General > Background App kisha chagua app ambazo hutaki zifanye kazi kwa wakati huo.
>Power Mode. Simu janja nyingi (kama si zote) huwa zinaarifu kwa taarifa fupi (notification) mara tu simu janja zinapofikia 15%-20% ya kiwango cha chaji na kama ukiweka simu yako katika mfumo inamaanishi matumizi ya betri yanapunguzwa sana kutokana na simu kuwa katika mpangilio wa power mode.
Kwa ambao vifaa vyao vinatumia iOS 11 inashauriwa kupunguza kiwango cha muda ambao kiasi cha betri kikifikia (kiwe juu ya 20%) ndio simu inakuwa kwenye mfumo wa power mode. Hali hii itasaidia kupunguza matumizi ya betri kwa kupunguza mwanga kwenye simu, kupunguza muda wa simu kujifunga yenyewe (pale inapokuwa haitumiki) na vilevile inasitisha programu tumishi zinazofanya kazi bila ya mtumiaji kuziruhusu.
>Zuia programu tumishi, SIRI isifanye kazi. Kama si mtumiaji wa app, SIRI mara kwa mara basi ni vyema ukaizuia isifanye kazi muda wote ili kufanya kifaa chako kiweke kikaa na chaji muda mrefu. Kuweza kuzima app SIRI isifanye kazi unaenda Settings>>Siri&Search kisha unazima kipengecle cha “Hey Siri”.
>Zuia ‘kisaidizi cha mguso’ (assistive touch) kisifanye kazi. Kipengele hiki ni muhimu sana pale unapoona uvivu wa kugusa sehemu fulani kwenye simu/iPad yako na basi yake ni kusaidia kuperuzi kwenye kifaa chako cha Apple mfano kupangusa kwenye kioo kwa kutmia kidole zaidi ya kimoja. Kuzuia assistive touch isifanye kazi ingia Settings > General > Accessibility > AssistiveTouch.
>Refusha muda wa barua pepe kuingia kwenye kifaa chako (iPhone/iPad). Matumizi ya barua pepe siku hizi yameongezekana sana kutokana na kwamba mtu haitaji kutumia kompyuta yake ili aweze kujibu ujumbe/kutuma barua pepe kwa kutumia kompyuta bali siku hizi kazi hiyo inaweza kufanyika kwa kutumia simu janja na kwa kutumia muda mfupi sana kufanikisha kutuma barua pepe.
Kitendo cha iPhone/iPad yako kuangalia mara kwa mara iwapo kuna barua pepe imeingia kinachangia kifaa chako kisikae na chaji kwa muda mrefu. Ni muhimu kuweka muda wa dakika 30 au zaidi kuweza kungualia kama kuna chochote kimpya kwenye barua pepe. Ingia Settings > Accounts & passwords > Fetch New Data kufanya mabadiliko.
Ni muhimu kuwa mwangalifu sana na simu yako ili kuhakikisha haizimi kabla ya ule muda ambao unakuwa karibu na chaji ya iPhone/iPad yako ili kuweza kuichaji hivyo maelezo na uchambuzi wa hapo juu uchukulie kwa uzito wa aina yake.
Vyanzo: News in color, Telegraph