fbpx
Facebook, whatsapp

Facebook Kuachana Na Mpango Wake Wa Kutaka Kuonesha Matangazo WhatsApp!

facebook-kuachana-na-kuonesha-matangazo-whatsapp
Sambaza

Facebook na WhatsApp ni mitandao ya kijamii ambayo ni mikubwa na yenye majina makubwa sana duniani. Ikumbukwe kuwa FB ndio inaimiliki WhatsApp baada ya kuinunua miaka kadhaa iliyopita.

Facebook iliinunua WhatsApp lakini baadhi ya wafanya kazi na waanzilishi walibakia katika kampuni. Baada ya muda kidogo kulianza kutokea tofauti za kiuongozi na kimaono, hali ambayo imepelekea waanzilishi hao kujivua na kampuni ya WhatsApp. Hii sio mbaya sana kwani waliuza kampuni hiyo kwa FB kipindi cha nyuma.facebook whatsapp apps

INAYOHUSIANA  WhatsApp kuja na muonekano wa giza

Vile vile Facebook ilitangaza kuwa itaanza kurusha matangazo (ya kulipwa) katika mtandao wa WhatsApp kupitia eneo la status. Hii ikiwa ni njia moja ya kwa Facebook kujihakikishia kuwa wanaongeza pato lao

Facebook vile vile walitangaza kuwa WhatsApp na FB ziwe na daraja ambalo linaunga mitandao hiyo miwili, japokuwa wazo hilo lilipigwa na wengi lakini bado lilifanikiwa. Sasa hivi unaweza post status WhatsApp na Facebook kwa wakati mmoja.

INAYOHUSIANA  Facebook Kubadilisha Sera ya Kutumia Majina Halisi

Licha ya hivyo inasemekana kuwa FB inajikita zaidi katika kuhakikisha watu wenye biashara zao kupitia mitandao hiyo wanakutanishwa vizuri na kwa ukaribu zaidi na wateja zao na jinsi ya kusimamia mawasiliano/mahusiano hayo.

facebook whatsapp
FB Ikiwa Imeimeza WhatsApp

KWA TAARIFA YAKO

  • Jarida la Wall Street limechapishwa kuwa timu ambayo ilibidi ifanye mchakato mzima imefutwa
  • Ile ‘Code’ ambayo waliiandika WhatsApp ili ifanye zoezi hili imefutiliwa mbali

Sawa plani za FB kutangaza kupitia WhatsApp pengine inaweza ikawa ndio tamati, lakini ambacho kinajilikana ni kwamba WhatsApp bado inatafuta njia ya kuweza kutangaza kupitia katika eneo lake la status.

INAYOHUSIANA  Facebook yalegeza masharti kuhusu matangazo ya sarafu za kidijitali

Soma Zaidi Kuhusu Facebook/WhatsApp

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika kibksi cha maoni. Umelipokeaje hili, Pia Usisite kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com