PlayStore Kutoonyesha Masasisho (Updates) Ya #App Tena Ktk Notification!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Google Playstore ambayo inapatikana katika programu endeshaji ya Android ambayo pia inamilikiwa na kampuni ya Google, imekuja na boresho au badiliko. Mabadiliko hayo wengi wameyapokea na kila mmoja ana lake la kusema kulingana na alivyo yapokea

Badiliko hili ni kwamba endapo App zitapata sasisho (Update) basi katika sehemu ya ‘notification’ haitaweza kuonesha kwamba App husika imepata sasisho. Zamani ilikua hivi; kwa mfano Apps zikiwa zinapata masasisho (updates) ilikua ni lazima uwezo kuona masasisho hayo katika eneo la ‘notification’.

apps za kuziondoa google playstore android

Muonekano Wa Soko La Apps La PlayStore

Msemaji wa Google aliweka wazi kuwa Playstore haitaonyesha tena kwamba App zinajifanyia masasisho katika uwanja wa notification. Vile vile hata kama watumiaji watafanya masasisho kwa kuchagua wenyewe (manual updates) ukiachana na yale ya moja kwa moja (automatic updates) bado wembe ni ule ule hawataweza kuona katika uwanja wa ‘notification’

INAYOHUSIANA  Apple waleta iPhone 6 & 6 Plus , Saa na Mfumo wa Malipo

Taarifa ambayo wataipata ni ile tuu ambayo itawaambia kwamba App inajipakua (install) na baada ya zoezi hili ujumbe huu utajifuta baada ya App kujipakua kikamilifu

Muonekano Wa Soko La Apps La PlayStore

Pengine labda Google wameliona hili kwa sababu watu wengi hawafuatilii ‘notification’ za aina hii! Hivyo basi wameona ni muhimu kuzifutilia mbali ili kupunguza mlolongo wa notification nyingi katika simu ya mtumiaji.

INAYOHUSIANA  Yanayojulikana Kuhusiana Na Samsung Galaxy Note 8 Mpaka Sasa!

Pengine kuwezeshwa kwa hili ni mpaka mtumiaji awe na toleo la juu kabisa la programu endeshaji ya Android.

Wewe hili umelipokeaje? ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini kwenye kisanduku cha maoni. Kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.