fbpx

apps, Maujanja, Teknolojia, whatsapp

Uwezo wa kuwasiliana na WhatsApp moja kwa moja

uwezo-wa-kuwasiliana-na-whatsapp-moja-kwa-moja

Sambaza

Katika maboresho ambayo yanafanyika kwenye WhatsApp kwa asilimia fulani yanatokana na maoni ya watu ambayo yanatolewa na watu kupitia vyanzo mbalimbali na mambo mengine yanategemea kitu gani kitawavutia watu.

Katika miaka ya karibuni tumeona watoa huduma mbalimbali wakitafuta njia ya kuwa karibu na wateja wao kuweza kupata maoni yao kuhusiana na kile ambacho tayari kinatumika na mifano ipo mingi tuu mathalani Tigo Tanzania, Tanesco, n.k.

INAYOHUSIANA  Fahamu Teknolojia Ya Infinix NOTE 7!

Ukitaka kuwasiliana na WhatsApp kwenye App Store au Playstore kisha ukashuka chini kidogo utakutana na sehemu ya kuandika maoni (ingawa si chanzo pekee cha kupokea malalamiko/maoni); hapo ndipo wahusika husoma na kuchakata hivyo kujua nini cha kuboresha/kuongeza kwenye programu tumishi husika.

>Wapo mbioni kujisogeza karibu kabisa na wateja wao kwa mujibu wa WhatsApp Beta 2.20.202.7 ambapo katika kilichoonekana ni kipengele kipya cha “Contact us” kwa maana ya kwamba mtu ataweza kuwasilisha mawazo yake (ushauri, malalamiko, n.k) moja kwa moja na kupata majibu baada ya kufanyiwa kazi.

>Baada ya mhusika kupatiwa majibu mazungumzo hayo yatafungwa; hii ikimaanisha mara baada ya swali lako kujibiwa na ukiwa huna cha ziada basi mazungumzo yatafutwa (namna ya kulinda faragha).

kuwasiliana na WhatsApp
Kipengele cha “Contact us”kama njia ya kuwasiliana na WhatsApp  mbioni kupatikana kwa watumiaji wote.

Kama wewe ni mvivu wa kutoa maoni yako kupitia Playstore/App Store basi unaweza kuyatuma kwa barua pepe support@whatsapp.com. Tuambie msomaji wetu umeipokeaje habari hii?

Vyanzo: Gadgets 360, WABetaInfo

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|