Hadi leo hii Dunia bado inahangaishwa na janga la virusi vya Corona ambalo bado limeendelea kughasrimu maisha ya watu siku hadi siku. Kutokana na utandawazi taarifa kuhusu ugonjwa wa homa kali ya mapafu unapatikana kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo YouTube.
YouTube ni moja sehemu ambapo watu wanaweza kupata taarifa, kujifunza, kuburudika, n.k aidha kwa njia ya picha jongefu au sauti+picha. HIvyo, ni wazi kuwa kuna vitu vingi tuu ambavyo vinapatikana huko lakini tusisahau kuwa kuna suala zima la virusi vya Corona mbapo watu mbalimbali wanatumia YouTube kuchapisha ya ukweli na hata yale yasiyo ya ukweli/kupotosha. Kufuatia hilo YouTube inakabiliana na machapisho hayo kama ifuatavyo:-
itakataza machapisho yote ambayo yanamkanganyiko wa taarifa zinazotolewa na Shirika la Afya Duniani au mamlaka za afya kutoka kwenye nchi,
kuondoa picha mnato zote ambazo zinasema kuwa kinga ya virusi vya Corona itamuua mtu, kumfanya mtu asiwe na uwezo wa kubeba mimba au serikali kutumia njia hiyo kuwawekea watu kadi (chip) ndani ya mili kwa ajili ya kupata taarifa.
Machapisho yote mabaya kwenye YouTube kuhusu virusi vya Corona kutupwa nje.
Tangu mwezi Februari mwaka huu YouTube imeondoa picha mnato zaidi ya laki mbili ambazo zilikuwa zinapotosha taarifa kuhusu virusi vya Corona. Kwa taarifa hii hatuna budi kuwa waangalifu kwa kile ambacho tunaweka kwenye chaneli zetu ndani ya YouTube.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
No Comment! Be the first one.