fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Apple Intel Teknolojia

Intel vs Apple kwenye prosesa, Mkurugenzi wa Intel asema bado wapo juu

Intel vs Apple kwenye prosesa, Mkurugenzi wa Intel asema bado wapo juu

tecno

Kuna kavita kachinichini ka Intel vs Apple, kitu kinachoonesha ni jinsi gani kwenye biashara marafiki wanaweza wakageuka na kuwa washindani ndani ya muda mfupi.

Mwishoni mwa mwaka jana Apple walitambulisha prosesa zao mpya zinazokwenda kwa jina la M1, prosesa hizi zinazotumika kwenye laptop zake zilisababisha waache kutumia tena prosesa za Intel kwenye matoleo yake yote yajayo ya laptop za Macbook.

Katika kuitambulisha prosesa ya M1 Apple walisema hakuna prosesa ya Intel inayoweza fikia ufanisi wa prosesa hii kwenye kompyuta za Macbook. Walifanya hivyo kwa kulinganisha moja ya toleo lao la Macbook likiwa na prosesa ya Intel na ukilinganisha na ikitumia prosesa ya M1. Walisema kwa wastani prosesa ya M1 inafanya laptop ya macbook Air kuwa na ufanisi bora za zaidi ya mara 3.5 wakati kwa Macbook Pro ni ufanisi wa mara 2.8 au zaidi (CP).

Mkurugenzi mpya wa Intel, Bwana Pat Gelsinger alishasema ya kwamba kampuni ya Apple haiwezi kuishinda katika teknolojia ya utengenezaji wa prosesa. Na katika kuonesha mfano tuu, wameonesha data za tafiti za ufanisi wa programu mbalimbali kati ya matumizi ya kwenye kompyuta ya Macbook inayotumia prosesa ya M1 na kulinganisha na kompyuta ya Windows 10 inayotumia prosesa za Intel iCore 7.

 

Katika data za utumiaji zinazojumuisha utumiaji wa kazi za kawaida na zile za uchezaji magemu kwa asilimia kubwa bado inaonekana ufanisi upo bora zaidi kwenye kompyuta za Windows 10 zinazotumia prosesa za Intel iCore 7 ukilinganisha na Macbook za prosesa za M1.

SOMA PIA  Apple yapunguza bei ya betri ya simu zake

Intel vs Apple : Nyeusi ni prosesa ya M1 wakati bluu ni Intel i7.

intel vs apple

Intel vs Apple : Ufanisi kwenye uchezaji magemu, nyeusi ni prosesa ya M1 wakati bluu ni Intel i7.

 

intel vs apple

Ufanisi kwenye matumizi ya programu mbalimbali

 

Kuna maeneo bado prosesa ya M1 ni bora sana. Prosesa hii ya Apple haitumii umeme mwingi na pia haipati joto ata kwenye utendaji mkubwa wa kazi – na suala hili linafanya kompyuta mpya za Macbook zenye M1 ziweze kufanya kazi nzito bila kupata joto sana au kupiga kelele. Pia bado prosesa za M1 za Apple si nzuri kwa watumiaji wa vioo/monitor zaidi ya mbili. Kwa sasa prosesa hiyo haina uwezo wa kuhimili ufanyaji kazi wa kompyuta ikiwa imechomekwa kwenye monitor nyingine ya ziada zaidi ya moja.

SOMA PIA  OnePlus 8T Pro kutoonekana tena mwaka huu

Hakuna ubishi kuna jambo zuri la kiushindani lililoletwa na ujio wa prosesa za M1. Kubadilika kwa uongozi wa Intel mwaka huu, kwa kuingia kwa mkurugenzi mpya, kuna onesha nia kubwa ya kampuni hiyo kubadilika. Makampuni ya utengenezaji kompyuta mengi yatakuwa yanategemea makubwa kutoka kwa Intel ili kuhakikisha kompyuta za Windows zinaendelea kuwa na ufanisi wa kushindana na za Macbook.

Chanzo: TheVerge na Intel
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania