fbpx

Apple, IPhone, simu, Uchambuzi

Katika iPhone 12 Apple wamekuja Kitofauti Zaidi. #Uchambuzi

katika-iphone-12-apple-wamekuja-kitofauti-zaidi-uchambuzi

Sambaza

Apple watambulisha simu mpya za iPhone 12 na 12 Pro, simu ambazo zinakuja na mabadiliko makubwa katika ubunifu na teknolojia uliofanywa na Apple ukilinganisha na matoleo ya iPhone zilizopita.

Matoleo manne ya iPhone 12:

  • Toleo la inchi 5.4, iPhone 12 Mini,
  • Toleo la inchi 6.1, iPhone 12 na 12 Pro
  • Toleo la inchi 6.7, iPhone 12 Max
iPHONE 12
Mlinganisho wa ukubwa wa simu hizi mpya, ukilinganisha na matoleo mengine kadhaa ya nyuma

Teknolojia ya 5G

Kuna matoleo ya simu nne katika familia ya iPhone 12 na simu zote zinakuja na teknolojia ya kisasa zaidi ya mawasiliano kwa sasa ya 5G. Teknolojia ya kasi ya intaneti baada ya 4G.

Teknolojia mawasiliano ya 5G imeanza kupata umaarufu na mataifa mbalimbali yanapambana kuhakikisha teknolojia hiyo inaanza kupatikana kwenye mataifa yao – teknolojia ya 5G inawezesha kasi ya intaneti ya hadi kiwango cha kudownload Gb 1 au zaidi kwa sekunde. Ikiwa ni kasi yenye ubora wa mara 10 hadi 100 ukilinganisha na teknolojia ya 4G.

Soma habari zinazohusu teknolojia ya 5G kwa kubofya hapa – Teknokona/5G

Ili kuweza kutunza chaji kwa muda mrefu simu hizi zitaweza kuhama kutoka 5G na kwenda 4G pale simu inapogundua hakuna huduma/apps inayohitaji intaneti ya kasi ya 5G kwenye simu yako.

INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy S8 na S8 Plus: Zifahamu simu mpya kutoka Samsung! #Uchambuzi

Muonekano

Hili ndio toleo la kwanza la iPhone katika miaka mitatu lilokuja na muonekano wa kitofauti zaidi. Pia katika kioo/display wametumia teknolojia ya kisasa zaidi kuifanya display hiyo kuwa ndio ngumu na salama zaidi dhidi ya kuvunjika kuliko simu nyingine yeyote iliyopo sokoni kwa sasa.

Teknolojia hiyo imeitwa Corning Glass – Ceramic Shield.

iphone 12
iPhone 12 ikiwa na iPhone 12 Mini

Simu za bei ya juu, 12 Pro na 12 Pro Max zimetengenezwa kwa kutumia Chuma cha Pua (stainless steel)wakati simu ya iPhone 12 imetengenezwa kwa alumini (aluminium).

Kamera

iPhone 12 Pro na 12 Pro Max zinakuja na kamera tatu, zenye teknolojia za utambuzi wa mazingira (depth mapping), AR na uwezo wa kupiga picha nzuri ata pale mwanga ukiwa mdogo. 12 Pro inakuja na pia na kamera ya lens ya ‘telephoto’ yenye uwezo wa optical-zoom wa 2.5X, wakati katika 12 Pro Max lens hiyo ni ya optical-zoom kiwango cha 5X. 12 Pro inakuja na uwezo wa kuzoom kidigitali mara 10, wakati 12 Pro Max inauwezo wa wa mara 12.

INAYOHUSIANA  Simu ya Freedom 251 - Simu janja ya bei rahisi zaidi, Kuanza kupatikana Juni 30
iphone 12 pro max tanzania
Pro Max

iPhone 12 na 12 mini zinafanana kwenye kila kitu kasoro tuu ukubwa, hivyo kwenye kamera zote zinakuja na kamera mbili za megapixel 12, ultrawide. Pia kwa sasa simu hizi pia zinakuja na uwezo wa Night Mode, uwezo huo wa kupiga picha kwenye eneo la giza bila uhitaji wa kuwasha taa/flash upo kwenye simu hizi zote.

Ujazo:

iPhone 12 na 12 Mini zinakuja katika ujazo wa GB 64, GB 128 na GB 256, wakati 12 Pro na 12 Pro Max zinakuja katika ujazo wa GB 128, GB 256 na GB 512.

Mfumo wa Kuchaji wa MagSafe

Kupitia utambulisho wa simu hizi pia Apple wamerudisha na kuboresha mfumo wao wa kuchaji kupitia teknolojia ya MagSafe. Teknolojia magsafe inayopatikana kwenye laptop inahusisha uwezo wa chaja kuganda katika eneo la kuchaji ili kuhakikisha usalama wa chaja yako. Ila kwa sasa wametumia teknolojia hiyo kwenye eneo la nyuma ya simu hiyo na kutengeneza chaja ya bila waya (wireless charger) inayokuja pia na teknolojia hiyo.

INAYOHUSIANA  Simu janja: Zifahamu Oppo A9 na A9x
kuchaji iphone magsafe
Chaja inayotumia teknolojia ya Magsafe

Chaja ya ‘wireless’ ya magsafe itaweza kuchaji hadi saa janja za Apple. Ila pia kutokana na uwezo wa teknolojia hii tusishangae kuona watu wengine wakitengeneza vitu mbalimbali kwa ajili ya iPhone vitakavyokuwa vinatumia teknolojia hii ya usumaku iliyopo nyuma ya simu hizi.

magsafe iphone
Teknolojia hii inaweza kutumika kwa kuwezesha vitu kama vile ‘macover’ nk kuweza kunasa kwa nyuma ya simu hiyo na hivyo kurahisisha utengenezaji wake

Bei.

iPhone 12 Mini itaanzia bei ya dola 699 za Kimarekani (Takribani Tsh 1,700,000/=), wakati iPhone 12 itaanzia dola 799 (Takribani Tsh 1,900,000/=). 12 Pro zitaanzia dola 999 (Takribani Tsh 2,320,000/=), wakati 12 Pro Max zitaanzia dola 1,099 (Takribani Tsh 2,550,000/=). Kumbuka kwa Tanzania gharama zitazidi hizo kutokana na sababu za kikodi na biashara.

Je una mtazamo gani juu ya simu hizi? Je una mtazamo gani pia juu ya ukuaji wa teknolojia ya kuchaji simu? Kwa mara ya kwanza mabox ya simu hizi yatakuwa madogo kwani hayatakuja na chaja wala earphones. Hivi ni vitu ambavyo mtumiaji atatakiwa kuvinunua kivingine.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*