fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

LG simu

LG kuachana na biashara ya simu janja

LG kuachana na biashara ya simu janja

Habari hii ianayohusu LG kuachana na biashara ya simu janja inaweza kuwa ni ya kuhuzunisha hasa kwa wale wateja ambao wamekuwa wakivutia na bidhaa hizo kwa miaka mingi tuu lakini wenyewe wameona inatosha sasa.

Mwanzoni mwa mwaka huu tuliandanika makala inayohusu LG kuachana na biashara ya simu janja na sasa suala hilo linakaribia kufikia ukomo kwani tarehe rasmi ya kufungasha virago imewekwa wazi. Kuanzia Julai 31, LG inatakuwa haijihusishi na biashara ya simu janja mpya ingawa itaendelea kufanya yafuatayo:-

  • LG wataendelea kuuza simu ambazo bado wanazo kwenye akiba yao na kuna uwezekano wa watu kuzinunua kwa bei ya punguzo,
  • kuendelea kutoa masasisho ya ulinzi kwa simu janja mbalimbali ingawa itakuwa ni kwa kipindi fulani tu na
  • kuendelea kutoa ushirikiano kwa watu wanaoshikirikiana nao (wabia), wasambazaji wa simu janja za LG katika kipindi chote chakufunga biashara ya rununu.
kuachana na biashara

LG wanaona imetosha sasa kwenye biashara ya simu janja.

Kinachofuata kwa LG

Kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Korea Kusini inasemaitaelekeza nguvu zao kwenye vifaa vinavyotumika kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme, kufanya nyumba ziwe na mfumo wa teknolojia, utengenezaji wa roboti, matumizi ya utashi usio halisi, kutoa suluhisho ya vitu kati ya biashara na biashara, huduma nyinginezo.

kuachana na biashara

Mwaka 1995, LG ndio walianza kutengeneza simu na 2013 ndio walitoa simu janja ya kwanza.

Wenyewe wanasema wataendelea kuonekana kwenye soko la ushindani kwani mambo yalivyo hivi sasa dunia inategemea intaneti hivyo itajikita huko mathalani vifaa vinavyotumia teknolojia ya 6G.

Vyanzo: Gizmodo, The Verge

SOMA PIA  Mauzo ya simu yashuka robo ya kwanza ya mwaka 2019
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] kote wanafahamu kuwa LG inajiandaa kufungasha virago kwenye biashara inayohusisha simu janja lakini jambo hilo si la kufurahisha hasa kwa wale ambao wanazipenda rununu […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania