Kampuni ya Apple inc ya nchini Marekani inayojihusisha na utengenezaji wa bidhaa mbali mbali za Teknologia ikiwa ni pamoja na simu zilizojipatia umaarufu mkubwa zilizopewa jina la iphone imekua na utamaduni wa wakuwaacha midomo wazi watumiaji wa bidhaa zao pamoja na wapinzani kila wanapotambulisha bidhaa au huduma mpya.
Tarehe 4 mwezi huu Apple waliitambulisha na kuinadi Simu ya iphone 4s, simu hiyo haitofautiani muundo na ile iliyoitangulia yaani iphone 4 isipokuwa features zake zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana kuanzia kwenye uwezo wa camera, kasi ya utendaji na hata mfumo “Operating System”.
Moja ya vitu ambavyo vimeteka hisia za wadau wa maswala ya Teknologia pamoja na wapenzi wa simu za iphone kwenye toleo hili jipya (iphone 4s) ni feature iliyopewa jina la “Siri”, hii ni software ambayo inamuezeja mtumiaji wa iphone kuipa maagizo simu yake kwa kutumia sauti (voice commands) kitu hiki si kigeni sana lakini uwezo wa kutambua maagizo na kuyafanyia kazi haujawahi kuwa wa kiwango cha juu kwa kiasi ambacho software ya Siri kwenye iphone 4s imefikia.
Unaweza kutumia Siri kuiagiza simu yako kwa kutumia sauti kufanya chochote ambacho iphone 4s ina uwezo wa kufanya kuanzia kwenye kupiga simu, kutuma ujumbe, kutuma barua pepe n.k, mbali na kutenda kile ulichoiagiza simu yako kufanya “Siri” inaiwezesha simu yako kukujibu kwa sauti na kukueleza kile kinachofanyika. Natumaini umeipata vyema “Siri”.
Endelea kutembelea blog hii ili upate kufahamu features nyingine nyingi za iphone 4s pamoja na mambo mengine mengi.
Afrika, Facebook, Tanzania, Youth
Utumiaji Wa Intaneti Kwa Vijana Tanzania…Je ni Facebook tuu?
Hilo jambo leo naacha kama swali tuu…ila nakaribisha mawazo yenu, nategemea kesho kuandika zaidi kuhusu hili jambo. Je vijana wa Tanzania wanaotumia huduma za...
Linux, Teknolojia, Ubuntu
Ubuntu 11.10 Imeiva!
Kwa sasa yamebakia kama masaa 48 hadi Ubuntu 11.10 ipate kuwa online kwa watu wote kudownload na kufanya upgrades kwa wale wanaotumia version zingine....
Teknolojia
Karibu Teknokona (Kona ya Teknolojia Tanzania)
Shukrani za dhati kwako kwa kuweza kutembelea blog hii na tunaomba radhi kwa kutokuwepo kwa makala wala habari yoyote kwa sasa,. Hii ni kwa...