Sifa ya simu nzuri ni kuwa na kipuri mama chenye uwezo wa kuifanya rununu kufanya kazi zake kwa ufanisi na bila kumfanya mtumiaji kusubiri kwa muda ili kitu fulani kiwe kimewezakana kufanyika.
Qualcomm wameendelea kutoa vipuri mama kutoka kizazi kimoja hadi kingine na mwaka huu wameshatangaza kuja na toleo jipya kwa maana ya Snapdragon 8 Gen 2 amabapo uzinduzi wake utafanyika kwa siku tatu! Wakati ambao Qualcomm ilikuwa inaweka wazi kuhusu ujio wa toleo jipya pia waliweka wazi vipuri mama vipya kwenye saa janja zao; Snapdragon W5 na W5+SoCs.
Uzinduzi wa Snapdragon 8 Gen 2 utafanyika Novemba 15-17 huko Hawaii-Marekani. Shughuli hii ambayo hufanyika kila mwaka na mara nyingi imekuwa ikifanyika mwezi Disemba lakini mwaka 2022 imekuwa ni tofauti kidogo ingawa litafikia Hawaii kama ilivyo kawaida.

Kwenye uznduzi huo pia inategemewa kutambulishwa vipuri mama mbalimbali ambavyo vitatumika kwenye simu janja mbalimbali. Halikadhalika, makampuni makubwa ambayo yanataka kutumia Snapdragon kwenye rununu zao wanapenda kufanya nao biashara kabla ya kifaa hicho kuzinduliwa.
Hadi sasa Qualcomm hawajaweka wazi simu janja ambazo zina kipuri mama Snapdragon 8 Gen 2 lakini ni wazi kuwa rununu yoyote ambayo itatumia kifaa hicho basi itakuwa ni yenye uwezo wa juu kwenye ufanisi wake wa kazi.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.