Kampuni ya Xiaomi wiki iliyopita ilitangaza simu zao mpya, aina ya Xiaomi 12S, Walitangaza matoleo matatu ya simu hizo, zikiwa ni Xiaomi 12S, Xiaomi 12S Pro pamoja na Xiaomi 12S Ultra. Malengo hasa katika matoleo hayo ni kuboresha kamera za simu zao, wakitumia msemo wa “Capture The Moment”, huku wakiweka wazi azimio lao la kutengeneza simu bora zaidi duniani, hata kuwapiku washindani hasa Samsung na Apple ambao kwa sasa ndio wanaoongoza katika utengenezaji na mauzo ya simu janaja duniani.
Kwa kuanza, toleo la kwanza, Xiaomi 12S. Hili ndilo toleo dogo zaidi kwa umbo. Lina skrini yenye ukubwa wa inchi 6.28, ikiwa na paneli ya AMOLED yenye ubora wa hali ya juu. Simu hii inatumia Chipset aiinaya Qualcomm Snapdragon 8+ Gen 1 ikiwa na mfumo wa Android 12 kutoka Google, ukiwa na mwonekano wa MIUI 13 juu yake uliobuniwa na Xiaomi.
Unaweza kuipata simu hii ikiwa na RAM ya GB 8 au 12, pamoja na uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu wa GB 128, 256 au 512. Ina kamera tatu nyuma, zikiwa na ukubw awa Megapixel 50, 13 na 5 na kamera ya mbele yenye ukubwa wa Megapixel 32.
Simu hii pia ina Betri yenye ukubwa wa 4500 mAh, ikiwa na uwezo wa kuchaji kwa waya kwa nguvu ya Watt 67, ikitumia dakikka 42 kujaa toka asilimia 0 mpaka 100, uwezo wa kuchaji bila waya kwa nguvu ya Watt 50, ikitumia dakika 57 kujaa toka asilimia 0 paka 100, na uwezo wa kuchaji vitu vingine bila waya (Reverse Wireless) kwa nguvu ya Watt 10.

Simu hii inatumia waya wa aina ya USB Type-C, ikiwa haina sehemu ya kuchomeka earphones. Ina uwezo wa kusapoti mawasiliano katika kasi ya 5G, ikiwa na huduma za juu kabisa za WiFi 6e pamoja na Bluetooth 5.2.
Simu hii itauzwa kwa bei ya Euro 570 (takribani Tshs 1,336,450/-)*, huku ikipatikana katika Rangi nne; Nyeupe, Kijivu, Zambarau na kijani.
Xiaomi 12S Pro ndio toleo linalofuata katika mpangilio wa matoleo hayo. Haiachani mbali sana na simu iliyopita kwa sifa, kasoro vitu vitu kadhaa kama Skrini, ambapo hii ina skrini kubwa zaidi, katika size ya inchi 6.73, panel i yake pia ina uwezo wa kupunguza ama kuongeza kasi ya taarifa kwa kutumia Teknolojia ya LTPO.
Kamera pia zina utofauti kidogo, ambapo katika simu hii, kamera zote za nyuma zina ukubwa wa Megapixel 50,
Betri yake pia ni kubwa kidogo, ikiwa na ukubwa wa 4600 mAh, ambapo iaweza kujacji kwa waya, kwa nguvu ya Watt 120 , ikijaa kwa muda wa dakika 19, na kuchaji bila waya kwa nguvu ya Watt 50, ikijaa kwa dakika 42. Sifa nyingine zote zilizobaki ni sawa na simu ya Xiaomi 12S.
Simu hii inapatikana katika rangi sawa na Xiaomi 12S na itauzwa kuanzia Euro 670 (takribani Tshs 1,570,700/-)*
Toleo kubwa zaidi, la Xiaomi 12S Ultra litakuwna na maala yakee binafsi kwa kuwa ndilo lililopewa nafasi kubwa zaidi katika Matoleo haya, likiw ana sifa mbalimbali za kipekee ambazo tutazitazama kwa undani zaidi.
*Bei hizo ni kutoka nchini China ambapo ni kiwandani, bei katika nchi nyingine yaweza kuwa juu kutokana na tozo za kodi na usafirishaji.
No Comment! Be the first one.