WhatsApp ndio mtandao wa kijamii wa kutuma na kupokea meseji za papo kwa papo ambao ndio maarufu zaidi na hiki ni kingine kipya kutoka kwao.
Vyanzo mbali mbali vinasema kuwa kipengele kinachokuja katika mtandao huo ni uwezo wa kuweza kuficha watu kuona kama uko ‘Online”muda huo.

Kwa mfano hivi hujawahi kukutana na ile hali mtu anakutumia ujumbe unaufungua, unausoma, tiki za bluu zinaonekana, humjibu na bado uko ‘Online’
Baadae mtu anakuja kukutumia ujumbe tena kukulalamikia kwanini humjibu wakati bado uko “Online”???
Moja kwa moja hapo kinachotokea ni kwamba aliona kabisa lile neno ambalo limejiandika ‘Online”. Sasa fikiria kwa sasa utaweza kabisa kuliepusha hilo swala.
Kwa sasa toleo la WhatsApp la majaribio lenye huduma hii linatumika, na baada ya majaribio kukamilika basi kila mtumiaji ataweza kufurahia huduma hii.
Kwa sasa watu watakuwa na uwezo wa kuweza kuzima au kuwasha lile enep la ‘last seen’ na hii inayokuja ya ‘online’
Kama utakua unasumbuliwa sumbuliwa sana na hutaki mtu kujua kama upo ‘online’ kwa muda huo huduma hii itakusaidia sana…..au pengine unaweza ukawa na sababu zako tuu 😂
Soma Kila Kitu Kuhusu WhatsApp >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment, je utukuwa mmoja kati ya wale watakao tumia huduma hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.