fbpx

Utoaji wa talaka kwa njia ya simu wakemewa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ndoa ni jambo la kheri na daima ni kitu ambacho kinakumbukwa lakini ikitokea muunganiko huo wa watu wawili (mke na mume) ukaingia dosari na hata kufikia hatua ya kutaka kutalakiana hapo kwa wengine simu inakuwa nyenzo muhimu.

Unaweza usiamini lakini ni vitu ambavyo vinatokea na badala ya kutumia kalamu na karatasi kuandika talaka au kutumia njia ya mahakama baadhi ya wanaume wameamua kutumia njia fupi; kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda kwa mkewe kwa maana ya kwamba ndio talaka yake hiyo.

Labda Tanzania bara visa hivyo havijaibuka lakini kwa Tanzania Zanzibar mambo hayo yapo mpaka Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto kutoka SMZ, Bi. Moudline Castico kukemea na kupiga marufuku kwa wanaume kutumia njia hiyo kutoa talaka kwa mkewe.

Kitendo hicho (utoaji wa talaka kwa njia ya simu) kinatafsiriwa kama uzalilishaji na kumkosea heshima mwanamke hata kama haihitajiki tena kwa mumewe.

Bi. Castico alilisitiza kuwa taratibu statiki zifuatwe pale wawili hao wanapoona wameshindwana na kuachana kwa wema bila kumdhalilisha mwanamke.

Utoaji wa talaka

Simu ya mkononi ikitumika kama nyenzo ya kuwasilisha ujumbe kuwa umetoa talaka kwenda kwa mwenza.

Teknolojia ni nzuri lakini daima inatupasa tuitumie vyema kwa manufaa yetu. Simu kutumika kutoa talaka haina mantiki na inakiuka tamaduni zilizokuwepo miongo na miongo iliyopita. Tuige vitu vizuri lakini pia tudumishe tamaduni zetu.

Chanzo: Mtanzania

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu imepotea tuma IMEI kwenda cop@vsl.net - Hii habari ni ya uongo, usifanye hivyo
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.