WhatsApp kupitia tovuti yake imetangaza kwa watumiaji wa programu hiyo pendwa, kwamba sasa imewezesha watumiaji hao kuweza kupiga simu kwa njia ya WhatsApp (video/sauti peke yake) kwa watu wanne kwa wakati mmoja.
Ujio wa kipengele hicho ulitangazwa tangu mwezi Mei mwaka huu katika mkutano wa Facebook F8. Mtumiaji wa WhatsApp ataingia katika WhatsApp yake na kumpigia simu ya video/sauti peke yake rafiki yake kisha kwa upande wa kulia juu ataona alama ya kitufe cha kumuongeza (add participant) mtu mwingine.
