fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Teknolojia whatsapp

Vikatuni vya Money Heist kwenye WhatsApp

Vikatuni vya Money Heist kwenye WhatsApp

Spread the love

Tamthilia ya “Money Heist” imetokea kukonga nyoyo za watu wengi duniani kote na kusubiri kwa shauku mwendelezo wake. Kwa upande mwingine WhatsApp wameona inafaa kutengeneza vikatuni vya waigizaji kwa kwenye tamthilia husika.

Leo Septemba, 3 2021 umetoka mwendelezo wa tamthilia “La Casa De Papel” (Money Heist) hii ni toleo la 5. Taarifa za ujio wake zimekuwepo kwa miezi kadhaa sasa na hatimae siku yenyewe imewadia na watu duniani kote wanaweza kufurahia tamthilia kupitia vyanzo mbalimbali kwani hakuna kusubiri tena.

SOMA PIA  Fununu kuhusu bei za iPhone 12

Katika kuwafanya watumiaji wa WhatsApp na wapenzi wa tamthilia hiyo vimetengenezwa vikatuni vya waigizaji mbalimbali wa Money Heist ambayo wengi wetu tumeshapata kuifuatilia tangu toleo la kwanza hadi 4 na ya tano imetoka leo tayari kwa kwenda kwa watazamaji ambao waliisubiri vya kutosha.

Money Heist

Kufurahia ujio wa toleo namba 5 la La Casa De Papel WhatsApp wametengeneza vikatuni mbalimbali vya waigizaji wa tamthilia hiyo.

Upatikanaji wa vikatuni hivi inabidi mtu anayevitaka basi avipakue ili viwepo kwenye WhatsApp yake na hatimae kuweza kuvitumia atakapohitaji. UKIBOFYA HAPA utaweza kuviona kisha kuvipakua.

Tuambie ewe msomaji wetu, umefurahishwa na ujio wa mwendelezo wa tamthilia iliyotokea kuteka macho, masikio ya watu wengi duniani kote? Naamini wikiendi yako itakuwa murua kabisa. Usiache kutufuatilia kila siku ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika.

Chanzo: WaBetaInfo

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania