Mwaka 2019, Motorola iliamua krudisha kwenye ushindani simu za “Razr” ambazo zilikuwa maarufu miaka ya 2000 lakini kutokana na ukuaji wa teknolojia simu hizo zikaja zikiwa zinaendana na kile ambacho soko linavutiwa.
Mwaka huu toleo jipya la Moto Razr lilitazamiwa kutoka lakini inavyoonekana ni kwamba suala hilo limesogezwa mbele na bado haijafahamika tarehe ambayo simu hiyo itatoka. Tayari kimeshafamika kuwa mwezi huu (Julai) au mapema Agosti tutaweza kuona simu janja Edge X30 na Edge 30 Pro.
Ingawa ujio wake umesogezwa mbele lakini kwa mujibu wa taarifa rasmi Moto Razr 2022 zinasema rununu hiyo imewekwa Snapdragon 8+ Gen 1. Halikadhalika, muundo wake utakuwa na utofauti kidogo na toleo la awali. Toleo hili ambalo lilikuwa litoke katika siku za usoni litakuwa ni la tatu baada ya lile la 5G ambalo lilitoka mwaka jana.
Fununu nyingine zinzoihusu Moto Razr ni maboresho kwenye ukubwa na ubora wa kioo, upande wa kamera ambapo inaaaminika kuwa kamera kuwa itakuwa na MP 50 na ya pili 32MP.
Simu hii ambayo haijulikani ni lini itatoka inaaminika kuwa itakuja na memori (RAM) ya hadi GB 12 huku diski uhifadhi wa hadi GB 512 kitu ambacho kinachagizwa zaidi na aina ya kipuri mama ambacho rununu husika imewekwa.
Kuhusu ni lini Razr 2022 itatoka inatupasa kuendelea kusubiri mpaka hapo mapya yatakapofahamika na hakika TeknoKona tutawahabarisha ipasavyo.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.