fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Facebook Messenger Teknolojia Telegram whatsapp

Programu tumishi-Telegram yashushwa mara bilioni 1 hadi sasa

Programu tumishi-Telegram yashushwa mara bilioni 1 hadi sasa

Spread the love

Telegram-prgramu tumishi ambayo si maarufu kama ilivyo kwa hizo nyingine ambazo tunazifahamu na pengine hili linaweza likakushangaza lakini ndio imekuwa ya kwanza kushushwa mara bilioni moja duniani kote.

Kwa mujibu zilizotolewa hivi karibuni na Sensor Tower zinaonyesha programu imeshushwa mara bilioni 1 duniani kote hadi sasa tangu ujio wake mwaka 2013. Telegram ndio imekuwa ya kwanza kufikisha namba hiyo hata kabla ya washindani wake wa karibu kabisa; Facebook Messenger, Instagram, WhatsApp na nyinginezo.

SOMA PIA  Tarehe ya kuzaliwa ni lazima kwenye akaunti ya Instagram

Telegram inaweza isiwe na watumiaji wengi kama ilivyo kwenye Facebook lakini ndio programu tumishi ambayo inabuni vitu vizuri kuanzia usalama wake lakini pia maboresho mbalimbali kama picha mnato za makundi, mfumo wa jumbe za sauti ulioboreshwa, uwezo wa kuonyesha watu vitu vyako sambamba na kutoa maelezo (kama ilivyo kwenye Skype, Zoom, n.k).

Katika mafanikio megine ambayo Telegram inajivunia ni kuwa ya kwanza kushushwa mara 214.7 milioni katika nusu ya kwanza ya mwaka 2021 ambayo ni sawa na 61% ya ongezeko la mwaka hadi mwaka. Mwaka 2020, katika kiupindi swa na hicho ilikuwa imeshashushwa mara 133 milioni-Sensor Tower.

mara bilioni 1

Telegram yashushwa mara bilioni 1: Telegram inashushwa mara nyingi zaidi ya wengine duniani kote kutokana na usalama, sera ya faragha kwa watumiaji wake.

Watumiaji wengi wa Telegram wapo wapi?

Takwimu za Sensor Tower zinasema watumiaji wengi wa Telegram wapo India kwa muktadha wa watumiaji wa intaneti wakiperuzi kwenye programu tumishi husika ambapo karibu 22% ya walioishusha tangu kuanzishwa kwake wapo huko (India). Nafasi ya pili wanashika Urusi (10%) halafu Indonesia (8%) inafuata. Kushushwa mara bilioni 1 haimaanishi kuwa ina watumiaji wengi kuzidi wengine; mapema mwaka huu Telegram ilifikisha watumiaji hai wa kila mwezi milioni 500.

SOMA PIA  PlayStore Kutoonyesha Masasisho (Updates) Ya #App Tena Ktk Notification!

Makampuni mengi duniani wana akaunti ya Telegram mahususi kwa ajili ya kuwasiliana na wateja wao waliopo nchi mbalimbali duniani. Tuambie je, wewe una akaunti ya Telegram? Unaizungumziaje programu tumishi kwa muda ambao umeishaitumia?

Vyanzo: Gadgets 360, 9to5Mac

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania