fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Teknolojia Telegram whatsapp

Progamu ipi ya kutuma ujumbe ni bora kwako? Whatsapp au Telegram?

Ni wazi kuwa Whatsapp au Telegram zina mitazamo tofauti kwa faragha ya watumiaji na data. Ikiwa wasiwasi wa faragha ni kipaumbele au watumiaji wanapenda kuepuka kawaida, basi Telegram inapaswa kuwa chaguo nzuri.

Walakini, inapaswa kusema kuwa WhatsApp haiko nyuma sana. Zote WhatsApp na Telegram zinajivunia sifa nyingi kama vile kutazama picha na matumizi ya stika lakini wakati huo huo, programu hizi za kutumiana ujumbe zina huduma tofauti. 

KWANINI TELEGRAM NI BORA KULIKO WHATSAPP?

Whatsapp au Telegram

 • Sehemu ya mazungumzo ina ulinzi maalum ambao unaruhusu watumiaji kuweka kipima muda kwenye ujumbe ili kujifuta baada ya muda maalum, 
 • Watumiaji wa Telegram pia hupokea taarifa zilizopigwa picha (screenshot) zilizochukuliwa, 
 • Telegram inaruhusu picha, ujumbe wa maandishi, faili za media na nyaraka kuhifadhiwa mbali (cloud storage) bila ya kuwa na hofu ya kupoteza kitu hata kama ukifunga akaunti yako na kurudi baada ya muda,
 • Uwezo wa kumtafuta mtu kwenye Telegram kwa kutumia jina maalum (username),
 • Kuhakikisha faragha ya nambari ya mawasiliano ya watumiaji, na jina la mtumiaji, watumiaji wa Telegram wanaweza kuzungumza na wengine kwenye programu hata ikiwa hawana nambari ya mawasiliano ya wengine, 
 • Kikundi ndani ya Telegram kinaweza kuwa na watu mpaka elfu tano, WhatsApp ni 256. Vilevvile, kwenye Telegram kuna chaneli ambazo zinaweza kuwa na idadi isiyo na kikomo ya wanachama,
 • Kiongozi wa kundi kwenye Telegram anaweza kuficha asiwe anaonekana kwenye orodha ya wana kikundi,
 • Inawezekana kuweka mpangilio wa mtu kupokelewa na ujumbe mara tu anapojiunga na kikundi kwa kutaja jina alilosajili kwenye Telegram,
 •  Telegram haihitaji mawasiliano kati ya simu na kompyuta ili mtumiaji aweze kupokea/kuona jumbe; programu tumishi ya kwenye simu na kompyuta vyote vinajitegemea katika ufanyaji kazi,
 • Uminywaji wa media katika Telegram pia unaruhusu watumiaji kuchagua ikiwa wanataka kuminya uwezo wa picha na video au kutuma zikiwa na uwezo wake uleule.

KWANINI WHATSAPP NI BORA KULIKO TELEGRAM?

Whatsapp au Telegram

 • WhatsApp kwa sasa inajivunia watumiaji hai bilioni 1.6 ikilinganishwa na Telegram iliyoripotiwa watumiaji milioni 200 kila mwezi. Hii inamaanisha marafiki na familia yako wana uwezekano mkubwa wa kuwa na WhatsApp badala ya Telegram, 
 •  Whatsapp imeweka ulinzi wa mawasiliano kati ya mtu na mtu wakati kwenye Telegram kipengele hicho ni mpaka mmojawapo awe ameanzisha mazungumzo ya faragha/siri, 
 • Whatsapp inaruhusu mtumaji kujua juu ya uwasilishaji na hali ya kutambua kama ujumbe ulifunguliwa.

Ndio hivyo tumewasilisha kwenu wasomaji wetu sasa ni mimi na wewe kuamua tunaegemea wapi au tunaendelea kutumia zote mbili kutokana na sababu mbalimbali zisizozuilika. Tupe maoni yako.

Vyanzo: Express UK, Siraj Abbas

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania