fbpx

Picha mnato kwenye IG zinaboreshwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wabunifu wa programu tumishi ya Instagram wanaonekana kuendelea kuweka nguvu zaidi kwenye vitu vinavyohisiana na picha mnato kwenye IG kwani kitu kizuri kinafanyiwa majaribio.

Ukianza kuchambua masasisho/vitu vivya vinavyohusiana na kipengeele cha picha jongefu ndani ya Instagram utakuwa si chini ya vitu vitatu mpaka sasa vimeshawekwa. Sasa ni zamu ya kitu kingine kizuri ambacho utaweza kusema “Mtu fulani yupo kwenye hicho (picha jongefu) ulichokichapisha”.

Katika kuiboresha IG baadhi ya watu hivi sasa wanaweza kutaja orodha ya watu walipo kwenye picha jongefu aliyoichapisha kwa Kiingereza inafahamika kama “Tagging“.

Utofauti wake kati kumuorodhesha mtu kwenye picha na picha mnato ni kutoonekana moja kwa moja majina ya watuhivyo itabidi kugusa kidogo kisha ukurasa utafunguka na utaona wale wote walioshirikishwa.

picha mnato kwenye IG

Kipengele hicho kipya kinatazamiwa kuja kuwavutia watu wengi mara kitakapoanza kupatikana kwa wote.

Ni kupitia kwenye simu tu ndio mtu ataweza kuona kama ameshirikishwa kwenye picha jongefu. Tunaopenda kutumia Instagram tumewekwa pembeni.

Vyanzo: TechCtrunch, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Amazon kuunda programu ya kujipima nguo
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.