Kuna tetesi kwamba kampuni nguli ya utengenezaji wa simu tableti na kompyuta ya Apple itaanza kutengengeneza vioo (screen) vyake kwa kutumia teknolojia ya OLED (Organic Light Emitting Diode), mpaka sasa vifaa vyote kutoka kampuni ya Apple vinatumia teknolojia ya LCD (Liquid Crystal Display).
OLED ni teknolojia ambayo hutumia organic compound kutoa mwanga pindi inapopitishiwa umeme, teknolojia hii inatumika kutengeneza screen za vifaa mbali mbali na makampuni kama vile Samsung na LG yamekwishaanza kutumia teknolojia hii katika vifaa vyao.
Kwa mujibu wa tetesiĀ kutoka Nikkei ni kwamba Apple wamekwisha anza taratibu juu ya kuanza kutumia teknolojia hii hata hivyo wawapenzi wa bidhaa za Apple watahitaji kusubiri mpaka mwaka 2018 ambapo ndipo wataweza kuanza kutumia vifaa vya Apple vyenye teknolojia hii ya OLED.
OLED ni teknolojia ambayo inasifa nyingi pamoja na kuwa nauwezo mzuri wa kutunza chaji, na muonekano mzuri wa picha. OLED imekuwa inakuwa kwa kasi na kuboreshwa kwa haraka zaidi kushinda LCD na pengine hii ndiyo sababu kwa Apple kuhamia mfumo huo.
Zipo simu nyingine nyingi ambazo vioo vyake vimetengenezwa kwa kutumia mfumo huu wa OLED, simu hizo ni kama Motorola X Force, Gionee S6, na Samsung Galaxy J3.
One Comment