Kampuni ya Huawei kwa muda mrefu imekuwa ikifanya jitihada ya kuteka soko la Marekani na hivi karibuni imefurahi mafanikio katika maeneo kadhaa ya Marekani kwa kuuza simu janja zake kwa wingi.
Hata hivyo inaonekana serikali ya Marekani itakuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa kampuni hiyo kuendelea kufanya vizuri na kusambaza simu zake katika soko la Marekani.
Ni kwamba wakuu sita wa ngazi za juu wa mashirika ya kipelelezi ya Marekani wamewaagiza wananchi wao kutotumia simu na vifaa kutoka makampuni ya Huawei na ZTE.
Viongozi hao wa juu wa mashirika ya kipelelezi yakiwemo ya CIA, FBI, NSA na wakuu wengine wameonekana kukubaliana kwamba bidhaa za Huawei sio za kuaminiwa na raia wa Marekani.
Mkurugenzi wa FBI Chris Wray alisema kuwa kutumia simu za mkononi za Huawei kutawapa uwezo kudhibiti na kuingilia juu ya miundo mbinu ya mawasiliano ya simu ya Marekani.
Mabosi hao wa mashirika ya kipelelezi ya Marekani wanasema ukaribu wa kampuni hizo na serikali ya China ndio unawatia wasiwasi wa kutoamini bidhaa zao kwa matumizi ya wamarekani.
2 Comments
Comments are closed.