fbpx

Simu mpya ya Samsung Galaxy S9 na S9 Plus hii hapa

0

Sambaza

Jumapili kampuni ya simu ya Samsung imetambulisha simu janja ya Samsung Galaxy S9 na Samsung Galaxy S9 Plus katika mkutano mkubwa unaojulikana kama Mobile World Congress (MWC) huko Uhispania katika jiji la Barcelona.

Samsung Galaxy S9 haina tofauti sana na Samsung Galaxy S8 lakini S9 imeboreshwa zaidi katika eneo la Kamera. Samsung Galaxy S9 imewawezesha watumiaji wake kuweza kuchukua picha bora zaidi hata katika mazingira yenye mwanga hafifu sana.

Aidha katika upande huo kamera wameweka kipengele cha Augmented Reality (AR) kama walivyofanya Apple katika iPhone X ambapo wanakiita AR Emoji kipengele hicho kinamuwezesha mtumiaji kupiga picha za Selfie zikiwa na muonekano wa Emoji.

INAYOHUSIANA  Oreo yafika kwenye Samsung Galaxy J7 Prime

Angalia sifa kamili za Samsung Galaxy S9 na Samsung Galaxy S9 plus.

Teknolojia ya mawasiliano:

2G bands GSM 850 / 900 / 1800 / 1900 – SIM 1 & SIM 2 (dual-SIM model only)
3G bands HSDPA 850 / 900 / 1700(AWS) / 1900 / 2100
4G bands LTE
Speed HSPA 42.2/5.76 Mbps, LTE-A (6CA) Cat18 1200/200 Mbps
GPRS: Ndio
EDGE: Ndio

Mfumo Endeshi:
Android 8.0 (Oreo)

Samsung Galaxy S9

Muonekano wa Samsung Galaxy S9

Uhifadhi:

RAM: 4GB na Ujazo wa ndani (Storage): 64/128/256 GB.
Eneo la memori kadi (External Storage): Unaweza kuweka mpaka memori ya ukubwa wa 400GB.

Prosesa:
10nm, 64-bit, octa-core processor (2.8 GHz Quad + 1.7 GHz Quad)

Kamera:

Kamera ya nyuma (Rear): 12MP.
Kamera ya mbele (Selfie): 8MP

INAYOHUSIANA  Samsung yaonyesha simu yake ya mkunjo itakavyokuwa

Ukubwa wa kioo-5.8-inch Quad HD+Curved Super AMOLED

Ujazo wa Betri

3000 mAh

Sifa ya Samsung Galaxy S9 Plus ni

Teknolojia ya mawasiliano:

2G bands GSM 850 / 900 / 1800 / 1900 – SIM 1 & SIM 2 (dual-SIM model only)
3G bands HSDPA 850 / 900 / 1700(AWS) / 1900 / 2100
4G bands LTE
Speed HSPA 42.2/5.76 Mbps, LTE-A (6CA) Cat18 1200/200 Mbps
GPRS Ndio
EDGE Ndio

Mfumo Endeshi:
Android 8.0 (Oreo)

Uhifadhi:

RAM: 6GB na Ujazo wa ndani (Storage): 64/128/256 GB.
Eneo la memori kadi (External Storage): Unaweza kuweka mpaka memori ya ukubwa wa 400GB.
Prosesa:
10nm, 64-bit, octa-core processor (2.8 GHz Quad + 1.7 GHz Quad)

INAYOHUSIANA  Samsung kuongeza ubora wa kamera

Kamera:

Kamera ya nyuma (Rear) zipo mbili: 12MP.
Kamera ya mbele (Selfie): 8MP

Ukubwa wa kioo-6.2-inch Quad HD+Curved Super AMOLED

Ujazo wa Betri-3,500 mAh

Simu hizi zitaanza kuuzwa mwezi Machi na makadirio ya bei ni kuanzia shilingi milioni 2.6 na kuendelea.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.