fbpx
Kompyuta, Samsung, simu, Teknolojia, Udukuzi

Ripoti: Samsung Galaxy S7 ina tatizo!

ripoti-samsung-galaxy-s7-ina-tatizo
Sambaza

Kama unatumia simu janja, Samsung Galaxy S7 unatakiwa ujihadhari na udukuzi kwani watafiti kutoka chuo kikuu cha Graz nchini Austria wamebaini kuwa simu hiyo ipo katika hatari ya kuweza kudukuliwa.

Siku si nyingi wanaomiliki simu janja hiyo walitahadharishwa kuwa simu zao zinaweza kudukuliwa kutokana na udhaifu uliobainika kitu ambacho mdukuzi anaweza akaingia kwenye simu hiyo na kujua vyote vilivyopo kwenye simu.

Tatizo hilo kwa lugha Kiingereza tunasema meltdown na kimsingi ni tatizo ambalo lilianza kuonekana kwenye vipuri vya Intel kwamba mdukuzi anakuwa na uwezo wa kuchungulia kwenye kipuri hicho na kuweza kuona taarifa.

Samsung waliweza kupewa taarifa na tangu hapo wamekuwa wakitoa masasisho ya kuifanya simu zote za Samsung Galaxy S7 kuwa imara na kutoweza kudukuliwa.

Samsung Galaxy S7
Smsung Galaxy S7 inaelezwa kuwa na watumiaji zaidi ya watu 30m duniani kote.

Watumiaji wote wa Samsung Galaxy S7 wameshauriwa kuhakikisha simu zao zina masasisho ya karibuni na kama hawajayapakua wafanye hivyo mara moja; settings>>about>>software update>>check for updates.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Facebook kuja na Mfumo wa Magemu - kama vile Steam
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Ripoti: Samsung Galaxy S7 ina tatizo! – TeknoKona Teknolojia Tanzania
    August 10, 2018 at 12:59 pm

    […] post Ripoti: Samsung Galaxy S7 ina tatizo! appeared first on TeknoKona Teknolojia […]