fbpx

Google ina kifaa chake cha kudhibiti udukuzi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wafanyakazi wa Google wamekuwa wakisumbuliwa sana na suala zima la watu kujaribu kuingia kwenye kompyuta zao ili kuweza kujua yaliyomo huko lakini sasa itabidi wafikirie zaidi kuweza kudukua.

Karibu na mwisho wa mwezi Julai 2018 Google waliweza kuzindua kifaa ambacho kazi yake ni kuhakikisha usalama wakati ma matumizi ya nenosiri/jina maalum (username) ambao utaweza kuingia kwenye mtandao/tovuti husika.

Kifaa hiki kutoka Google kinaitwa Titan Key ambapo kipo katika mfumo wa USB na kazi yake ikiwa ni kufanya umadhubuti wakati mtu anapojaribu kuingia ukurasa wa barua pepe, Facebook, Twitter au sehemu nyingine ambayo itamuhitaji kutumia nywila/barua pepe.

Titan Key inaelezwa kuwa bora zaidi kwa ile teknilojia ya kutumia njia mbili za kuthibitisha kuwa hiyo kweli ni akaunti yako (two-factor authentication) kwa sababu ya kutohitaji kupokea ujumbe ili kuweza kuingiza tarakimu fulani.

kudhibiti udukuzi

Titan Key: Kifaa kilichotengenezwa na Google kuweka ulinzi madhubuti tunapoingia kwenye akaunti zetu mbalimbali.

Kifaa hicho kinakuja katika aina mbili; moja unaweza ukachomeka kwenye kompyuta na kingine kinafanya kazi kwa njia ya Bluetooth hivyo kuweza kutumika kwenye simu janja na kudhibiti udukuzi.

Sio vitu vya kufikiria kuvipoteza kwani vinginevyo hutaweza kuingia kwenye akaunti zako na bei yake inaelezwa kuwa ni $20|Tsh. 46,000 kwa kuagiza.

Vyanzo: Engadget, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Google kuendelea kushirikiana na Huawei kwa siku 90 zijazo
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|