Uvujishaji wa taarifa mbalimbali ni tatizo linalozikumba sekta mbalimbali hasa upande wa teknolojia kutokana na sekta hiyo kuwa na mvutano mkubwa wa kibiashara pamoja na sababu nyingine kadhalika.
Apple wanatambulisha iPhone 8 ikiambatana na iPhone 7s na 7s plus leo Septemba 12, 2017 lakini mambo yamekuwa si shwari baada ya taarifa nyeti kuhusu bidhaa mbalimbali kuvuja kabla ya siku ya uzinduzi.
Taarifa zilizofichuliwa ni za simu ya iPhone X pamoja na ya simu mbili aina ya iPhone 8 na inadaiwa ndio uvujaji mkubwa zaidi kuwahi kutokea.
Imebainika kuwa mtu asiyejulikana alichapisha anwani za iOS 11 zinazofahamika kama Golden Master (GM) ambazo zilifungua teknolojia katika kompyuta za Apple.
Hata hivyo taarifa kuhusu vifaa vipya vya Apple zlifichuliwa mwezi Agosti na kuonekana uvujajaji huo ulifanyika kimakosa. Imedaiwa uvujaji huo wa taarifa kutoka Apple wa hivi majuzi ulikwa wa makusudi.
Kuvuja kwa taarifa mbalimbali ni wazi kuwa kunaichafua kampuni husika jambo linaloweza kupelekea kutoelewana wenyewe kwa wenyewe ndani ya kampuni na ni ni wakati sasa kwa makampuni kuhakikisha inajidhatiti kuhakikisha taarifa hazivuji.
Chanzo: BBC