fbpx
Google, Magari

Magari yanayojiendesha yenyewe bila dereva ndani kupata ruhusa California

magari-yanayojiendesha-yenyewe-bila-dereva-ndani-california
Sambaza

Serikali ya jimbo la California nchini Marekani imesema inategemea uwepo wa magari yanayojiendesha yenyewe bila dereva ndani kufikia mwezi Aprili mwaka huu.

Kwa muda mrefu makampuni yanayofanya majaribio ya magari yanayojiendesha yenyewe yamekuwa yakikutana na hitaji la kisheria la Calfornia ya kwamba lazima ndani ya magari hayo kuwe na dereva mwanadamu – kama ‘backup’, kama ikitokea mfumo wa kujiendesha wenyewe ukiwa na hitilafu.

Magari yanayojiendesha yenyewe bila dereva ndani kupata ruhusa California
Gari linalojiendesha lenyewe na huku likiwa halina usukani, likiwa katika maonesho. Hili limetengenezwa na Google

Ila sasa serikali hiyo imekubali kukubali utumiaji wa teknolojia ya ‘remote human operator’, yaani kuwa na mtu aliyekwenye kituo flani akiwa na uwezo wa kufuatilia gari linalojiendesha lenyewe kupitia huduma ya intaneti na hivyo kuweza kulipokonya gari hilo uendeshaji na mtu huyu kuweza kuliendesha gari hilo ingawa yupo sehemu nyingine kabisa.

INAYOHUSIANA  Shiriki Olimpiki ndogo iliyoanzishwa na Google! #Gemu

Hitaji hili ni muhimu kwa makampuni yanayotengeneza magari yanayojiendesha yenyewe kama Google kupitia kampuni yake ya Waymo, na pia kampuni ya General Motors, ambao wote wanalenga kuweza kuyauza magari hayo ata kwa makampuni yanayotoa huduma za taksi kama vile Uber.

Gari linalojiendesha lenyewe
Gari linalojiendesha lenyewe, hili limetengenezwa na kampuni ya Waymo

Uwepo wa magari haya inamaanisha makampuni ya huduma za taxi yataweza kupunguza gharama kwa kuondoa uhitaji wa madereva katika magari na hivyo mtu mmoja atakayekuwa ofisini atakuwa na uwezo wa kufuatilia ata magari 5 – 6 yanayojiendesha yenyewe na kuingilia kati kama mfumo (AI – Akili feki ya gari) itakuwa na shida.

INAYOHUSIANA  Sasa Utaweza Kutumia Akaunti ya Google bila Password (Nywila)

Teknolojia ya ‘remote control’ kwa vifaa kama magari tayari inatumiwa na mashirika mengine Marekani kama vile NASA na jeshi la nchini Marekani.

Google na General Motors si makampuni pekee yanayotarajiwa kunufaika na mabadiliko haya ya sheria kwa jimbo la California, wengine watakaonufaika ni pamoja na Nissan, Waymo, Phantom Auto na mengine mengi yanayojihusisha na teknolojia za magari yanayojiendesha.

Chanzo: TheDrive na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |