Watu wengi duniani hivi sasa wanatumia sana WhatsApp kufanya mawasiliano na ndugu, jamaa na hata marafiki kwa kutumia simu janja au kwenye wavuti (WhatsApp Web). Je, wewe ni kati kati ya wale wanaotumia simu janja ambazo zinatumia Android 4 au iOS 9 kushuka chini?
Wapo watumiaji wa rununu ambao si wapenzi wa kubadilisha baada ya mwaka, miaka miwili, mitatu au hata mitano na zaidi kupita kutokana na sababu mbalimbali ambazo siwezi kuziongelea lakini mtu/watu hawa wanajikuta kwamba simu zao haziwezi tena WhatsApp mara tu alipata ujumbe kuwa nanukuu kwa tafsiri isiyo rasmi “…….toleo hili la WhatsApp limepitwa na wakati. Tafadhali imefanyie masasisho“.
Mtumiaji huyu anafuata maelekezo na kwenda kupakua maboresho kutoka App Store au Playstore kulingana na simu anayotumia kisha anakumbana na ujumbe unaosema “Toleo hili la WhatsApp haliendani na kizazi cha programu endeshi ndani ya simu yako” jibu ambalo linamfanya mhusika kuwa na maswali kadhaa asiyoweza kupata majibu ya papo kwa papo. Mimi kama mfuatiliaji wa masuala ya teknolojia jibu ya swali kwenye kichwa cha habari.
Kwa mujibu wa tangazo ambalo lilitoka Desemba, 30 2019, wahusika waliweka tangazo kwamba hadi kufikia Februari, Mosi 2020 wataacha kuendelea kuifanya WhatsApp itumike wenye simu za Android chini ya 4.0.3 (Ice Cream Sandwich) au iOS 9 kurudi nyuma. Kitu ambacho kimeshatekelezwa!.
Wala usione simu yako ni mbovu la hasha! Bali wameona vifaa hivyo ni vya muda kwa wao kuendelea kupeleka masasisho kwao. Kwahiyo kitu cha kufanya ni kutumia rununu zenye matoleo yanayoendana na waraka husika ili kuweza kutumia WhatsApp.
Vyanzo: GSMArena, Android Central