fbpx
Maujanja, Mitandao ya Simu, Tanzania, Teknolojia

Matumizi ya kidijitali kuepukana na virusi vya Corona

matumizi-ya-kidijitali-kuepukana-na-virusi-vya-corona
Sambaza

Virusi vya Corona vimekuwa tishio kwenye mataifa mengi duniani ikiwemo Tanzania na hali hiyo imesababisha shughuli mbalimbali kusitishwa angalau kwa kipindi cha mwezi mmoja lakini janga hilo halijatuzuia kutumia vifaa vyetu vya kidijiti. Je, tutasalimika?

Ni siku mbili sasa tangu taifa la Tanzania kupitia mamlaka husika itangazwe kuwepo na wagonjwa wenye virusi vya Corona ambavyo vinababisha homa ya mapafu inayoweza kusababisha kifo iwapo kinga ya mwili wa binadamu itazidiwa nguvu na adui huyo hatari. Tayari tumesahafamishwa njia mbalimbali ambazo tumeaswa kuzitumia ili kujikinga kupata maambukizi lakini hata kuzuia wengine kuambukizwa lakini matumizi ya kidijiti yanaweza kuzuia/kusambaza kwa tatizo lililoikumba nchi yetu.

INAYOHUSIANA  Mtandao wa SMART waongeza minara ya 4G Dar es Salaam

TeknoKona tumeamua kuja na makala hii ambayo tuna imani tutatumia simu zetu, vipakatalishi kwa namna ya kipekee ili basi tusiweze kuathiriwa na ugonjwa huo ambao umeshakatisha maisha ya maelfu duniani. Ongeza kasi ya matumizi ya kidijiti kwa manufaa yako:

 1. Fanya miamala kwa njia ya kieletroniki. Ni vyema tukawa wapenzi wa kutumia TigoPesa, HaloPesa, Airtel Money, n.k au hata benki mtandao kuweza kufanya manunuzi/malipo ya vitu mbalimbali jambo ambalo linafanya kitendo cha kufanya malipo kwa pesa mkononi ili kupata huduma hivyo kuepuka watu kugusana.
  Virusi vya Corona
  Tunaweza kufanya malipo kwa kutumia simu kama namna mojawapo ya kuepukana na virusi vya Corona.

  2. Usipende kusika simu/kifaa cha kidijiti ambacho si chako. Wakati huu si wa kuaminiana kuwa mwenzangu hana virusi vya Corona basi itakuwa si vibaya nikitumia simu yake au kifaa kingine cha kidjiti kwa lengo la kufanya mawasiliano ama kwa sababu nyingine kwani haujui kifaa hicho ni kisafi kiasi gani kutokuwa na vrusi hivyo. BOFYA HAPA kufahamu namna ya kufanya kifaa chako kiwe kisafi.

  Virusi vya Corona
  Kifaa chako kisiwetumiwe na wengi ili usije ukaugua na kupoteza nguvu kazi.

Watanzania tujiadhari na hili janga lililoingia nchini kwa kuweza kujikinga kwa kutumia mbinu ambazo tumeshazikia/kuziona kupitia vyombo mbalimbali vya habari lakini vilevile vifaa vyetu tunavyotumia kufanya mawasiliano na kupata habari tuvitunze na kuvilinda visije vikatuatuumiza.

Facebook Comments

Sambaza
2 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

2 Comments

 1. Matumizi ya kidijitali kuepukana na virusi vya Corona – Huduma
  March 18, 2020 at 8:51 pm

  […] post Matumizi ya kidijitali kuepukana na virusi vya Corona appeared first on TeknoKona Teknolojia […]

 2. Elimu kuhusu COVID-19 kupitia WhatsApp - TeknoKona Teknolojia Tanzania
  March 21, 2020 at 8:20 pm

  […] Matumizi ya kidijitali kuepukana na virusi vya Corona […]