Skype ambayo inamilikiwa na Microsoft imeingia mkataba na kampuni ya Paypal ambayo ni kampuni ya kimarekani inayojihusisha na malipo ya mtandaoni pamoja na kutuma hela duniani.
Mkataba huu utapelekea watumiaji wa Skype kutoka nchi 22 (kwa kuanzia ) kuweza kutumiana pesa moja kwa moja kutoka katika mtandao huu wa kupiga simu.
Ni wazi kwamba kampuni ya Microsoft ambayo ndiyo mmiliki wa Skype inataka kujiweka katika ushindani dhidi ya makampuni makubwa kama Facebook na Apple ambayo tayari yamekwisha ingia katika huduma za kimalipo za mtandaoni.

Mkataba huu utawawezesha watumiaji wa Skype kutuma pesa moja kwa moja kutoka katika app yao. Hata hivyo kwa kuanzia huduma hii itapatikana kwa watumiaji wa nchi 22 pekee ambazo ni Marekani, Uingereza, Austria, Ubeligiji, Kanada, Cyprus, Estonia, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Ireland, Italia, Latvia, Luxembourg, Malta, Uholanzi, Ureno, San Marino, Slovakia, Slovenia and Hispania.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kwamba Skype wameanza na huduma hii katika nchi ambazo kunawatumiaji wengi zaidi wa mtandao huo, hii inamaana kwamba iwapo huduma hii itaonesha mafanikio katika nchi hizo itaweza kusambazwa katika nchi nyingine (na pengine baadhi ya nchi za Afrika)
Kwakuwa kwa nchi kama Tanzania huduma za kipesa kwa njia ya simu kama vile Airtel money ndio zinafanya vizuri zaidi basi kunauwezekano mkubwa makampuni kama Facebook na Skype yakajaribu kuingia katika upande huu wa biashara kwa maeneo haya.