fbpx

apps, Teknolojia, whatsapp

Elimu kuhusu COVID-19 kupitia WhatsApp

elimu-kuhusu-covid-19-kupitia-whatsapp

Sambaza

Hivi sasa ulimwenguni habari ni kuhusu COVID-19 ambavyo vinasababisha homa ya mapafu na kuweza kusababisha kifo. Dunia ya leo ipo “Kiganjani” hivyo watu wana uwezo wa kupata taarifa mbalimbali wakiwa popote na muda wowote kupitia WhatsApp.

Watu wengi sana wameshapoteza maisha yao kutokana na homa kali ya mapafu inayosababisha na virusi vya Corona aina ya COVID-19. Sasa njia mbalimbali zinatumika kukabiliana na janga hilo lililoikumba dunia bila kusahau elimu kwa umma ili kuweza kuutokomeza hatimae hali irudi kuwa kawaida kwa kuondokana na tatizo hili.

SOMA PIA  Instagram Wabadili Maamuzi!

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa namba maalum ambayo watu wanaweza kuwasiliana nao kupitia WhatsApp wakati wowote ili kuweza kupata elimu, taarifa mbalimbali kuhusu virusi vya Corona. BOFYA HAPA kuweza kuanzisha mazungumzo ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu virusi vya Corona.

COVID-19
Elimu kuhusu virusi vya Corona (COVID-19) kupitia WhatsApp: Ili kuanzisha mazungumzo mtu ataandika neno “Join” au “Hi” kisha atajibu kwa kuandika namba/kikatuni (emoji) ya kipengele husika ili kuweza kupata maelezo.

Kupitia hapo watu wataweza kupata mengi kutoka shirika lenye dhamana ya kushughulikia afya duniani. Kwa hatua hii ina maana watu wanaweza kupata vitu vingi na vya uhakika kutoka kwenye chanzo cha kuaminika lakini pia tusipuuze taarifa zinazotolewa na WIZARA YA AFYA kuhusu virusi hivyo.

Vyanzo: GSMArena, WHO

Facebook Comments

Sambaza
2 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

  2 Comments

  1. Watu 12 kuweza kujumuika kwenye Google Duo - TeknoKona Teknolojia Tanzania
   March 28, 2020 at 1:51 pm

   […] Elimu kuhusu COVID-19 kupitia WhatsApp […]

  2. Watu 12 kuweza kujumuika kwenye Google Duo – Huduma
   March 28, 2020 at 2:47 pm

   […] mawasiliano ya kupitia picha jongefu (mnato/video) lakini wakati huu ambao dunia inapambana na virusi vya COVID-19; teknolojia hiyo ndio mkombozi wa wengi ukiacha Skype, WhatsApp na hata kwenye Google […]