fbpx
Facebook, India, Mtandao wa Kijamii, Teknolojia

Facebook waanzisha uwezo wa kufungua wasifu

facebook-waanzisha-uwezo-wa-kufungua-wasifu
Sambaza

Kwenye dunia iliyotawaliwa na utandawazi kwa kiasi kikubwa kwebye mataifa mengi hakika kuna mengi yanatokea kutoka kila pembe ya ulimwengu na hivi kuna mitandao ya kijamii basi imekuwa ni rahisi kufahamu mengi; yawe ya ukweli au uwongo vyote vinapatikana lakini umesikia kuhusu uwezo wa kufunga wasifu?.

Facebook ina watumiaji zaidi ya bilioni moja na wote hao wanatumia mtandao huo wa kijamii kuweza kufanya mawasiliano, kujua fulani kachapisha nini kwenye akaunti yake, n.k lakini kuna wengine faragha kwao ni kitu muhimu sana hasa kwenye ulimwengu uliojaa kila aina ya mazuri/mabaya. Hapo ndipo kipengele cha “Kufunga wasifu” kwenye Facebook kinakuwa na mantiki.

INAYOHUSIANA  Zijue Apps Za Picha Na Video Ambazo Ni Mbadala Kwa Instagram Na SnapChat!

Nini maana ya “Kufunga wasifu” kwenye Facebook?

Kwenye Facebook kuna kurasa inayoitwa “Profile” ama kwa tafsiri iyo rasmi “Wasifu”. Nikuulize ni mara ngapi umewaza kuwa na uwezo wa kufanya yale uliyoyaweka kwenye huo ukurasa (wasifu) ili watu waweze kufahamu wewe ni nani? Unaishi wapi? Ulisoma/unasoma shule ama chuo gani? Pamoja na mengineyo visionekane kwa wengine hasa ambao hawapo kwenye orodha ya marafiki zako kwenye Facebook?

INAYOHUSIANA  Microsoft: Serikali inachoifanyia Huawei si sawa

Sasa Facebook wameanzisha kipengele hicho kipya huko nchini India ambapo kwa yeyote ambae si rafiki yako huko hawezi kukuza, kupakua picha zako, kuona machapisho ya karibuni na hata ya zamani. Kipengele hiki kimeanzia huko India hasa kikiwalenga wanawake ambao wamedai kuwa wanataka kuwa na uwezo maradufu wa kuwa na faragha kwenye Facebook.

Kufunga wasifu
Facebook waboresha ulinzi wa taarifa za watu kwa kuweza kufanya wasifu wa mhusika usiweze kuonekana kwa kilka mtu.

Kipengele hicho kinaweza kisiwe kipya sana lakini bora zaidi kulinganisha na kilichopita cha “Profile Picture Guard” (ulinzi wa picha ya utambulisho) ambacho kilitoka karibu miaka mitatu iliyopita. Ndani ya siku chache zijazo kinaweza kuanza kupatikana kwa watumiaji wote wa Facebook. Vipi wewe umefurahishwa na kitu hicho?

Vyanzo: Gadgets 360, The India Express

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|