fbpx
Apple, iOS, iOS 12, IPad, IPhone, simu, Teknolojia

Kuna iOS 12.4.7 kwa ajili ya iPhone na iPad za zamani

kuna-ios-12-4-7-kwa-ajili-ya-iphone-na-ipad-za-zamani
Sambaza

Waswahili husema “Kipya kinynemi, ingawa kidonda” na “Usiache mbachao, kwa msaala upitao“. Ni misemo miwili ambayo naweza kulinganisha na jinsi ambavyo Apple wanatoa masasisho ya programu endeshi kwa iPhone na iPad za zamani.

Kutokana na sababu mbalimbali unaweza ukawa mpaka sasa bado unatumia iPhone 5s, 6, iPad (kizazi cha kwanza) ama kwa lugha nyingine bidhaa za Apple ambazo haziwezi kupokea iOS 13 (hivi sasa imefikia iOS 13.5 na imeshatoka!). Hilo lisikuhuzunishe sana kwani kampuni hiyo bado imeendelea kuzikumbuka bidhaa zake ambazo ni za muda kidogo na hivi sasa wanaweza kuhama toleo la nyuma kisha kwenda iOS 12.4.7.

INAYOHUSIANA  Simu ya mkononi ya kwanza kuwa na kamera
 iPhone na iPad
Toleo la iOS 12.4.7 laruhusiwa kupatikana kwenye iPhone/iPad za zamani.

Je, ni toleo gani za iPhone/iPad zinaweza kupaka sasisho hilo?

Kama ambavyo nilikuwa nimegusia kidogo tuu kuhusu rununu ambazo zimelengwa hapa zinakwendwa kwa mtiriko huu: iPhone 5s, 6, 6 Plus, iPad Air (kizazi cha kwanza), iPad mini 2, 3 na iPod touch (kizazi cha sita). Unakwenda kwenye mpangilio (settings)>>General>>Software update. Kisha subiri kwa sekunde kadhaa huku ukiwa umeruhusu intaneti lakini kumbuka kuwa na MB 100 ili kuweza kupakua sasisho hilo bila wasiwasi wowote lakini pia hakikisha kifaa chako kina umeme 50% au zaidi.

INAYOHUSIANA  Huawei P9: Huawei waomba radhi baada ya kupost 'uongo'!
 iPhone na iPad
Bidhaa mablimbali za Apple zilizoruhusiwa kupakua iOS 12.4.7.

Ni ushauri tuu kwamba kumbuka kupakua maboresho hayo na si kwenye bidhaa za Apple tu bali hata kwenye Android kwa usalama wa kifaa chako cha kiganjani. Daima usiache kutufuatilia kwa habari kadha wa kadha zinazohusu sayansi na teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, OSX Daily

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|