fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Tecno Uchambuzi

Uchambuzi wa Tecno Spark 5, Uwezo na Sifa.

Tecno Spark 5 ni mojawapo kati ya simu toka kampuni ya Tecno ambayo ina thamani nzuri kwa gharama yake ya manunuzi.

Kama kawaida kwa kampuni ya Tecno, huduma yao kuu ni kwa wateja wa viwango vya chini na kati na simu hii ni moja kati ya machaguo mazuri kwa kundi hilo. Kutokana na ukuaji wa teknolojia Tecno wanaendelea kutoa rununu ambazo zinaendana na mahitaji ya soko ikilenga ushindani wa kibiashara lakini pia kuzidi kuvutia wateja wengi zaidi sehemu nyingi duniani.

SOMA PIA  Fairphone: Simu janja inayoruhusu ubadilishaji wa vipuli kwa urahisi

Unafahamu undani wa rununu husika? Soma makala hii ili kuweza kupata majibu ya maswali ambayo umekuwa ukijiuliza kuhusiana na bidhaa husika. Sifa za Simu hii ya Tecno Spark 5 ni:

  • Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inch 6.6.
  • Mfumo Endeshi wa Android 10.
  • RAM ya GB mbili na diski uhifadhi ya GB 32.
  • Mfumo wa Camera nne nyuma (13 MP, 2 MP, 2 MP na QVGA) pamoja na Camera ya 8 MP mbele.
  • Betri yenye uwezo wa 5000 mAh.
  • Simu hii inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G, pia WiFi na Bluetooth, bila kusahau huduma ya redio. Spark 5
SOMA PIA  Simu janja ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya utengenezaji magemu

Pia, simu hii ina sehemu ya kutambua alama za vidole, sehemu ya kuchomeka earphones na sehemu ya kuchomeka waya wa kuchaji simu aina ya microUSB 2.0. Huja katika matoleo ya rangi mbalimbali, kama vile Kijani, Chungwa, Bluu na Kijivu. Bei yake ni zaidi ya Tsh. 400,000

Chanzo: GSMArena

SOMA PIA  Samsung kwa mwaka 2018: Kuuza mamilioni ya simu, Galaxy S9 ipo njiani

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania