fbpx

Tanzania, Teknolojia

Kushoto ni TEHAMA halafu kulia kuna VIRUSI VYA CORONA

kushoto-ni-tehama-halafu-kulia-kuna-virusi-vya-corona

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ina nafasi pana tuu katika vita hii dhidi ya virusi vya Corona ambapo jitihada na nguvu nyingi vimewekwa hapa lakini kinachotoka bado kinakuwa na njia mbili!

Mimi kama mwandishi na mfuatiliaji wa habari mbalimbali (ndani na nje ya Tanzania) napata shida sana kujua nafasi ya vyombo vya habari (runinga, magazeti, tovuti, n.k) pale inaposhindwa kutoa kitu kinachostahili. Hili limenikuna na nikiwa sehemu ya vile ambavyo nimevitaja nimeona niliseme. Nimekataa kuchukua njia ya kushoto/kulia ila nasimama palipo sahihi!

Tangu vita dhidi ya virusi vya Corona ni wanahabari/vyombo vya habari vichache sana nchini Tanzania wanaoweza kutambua janga hili kama VIRUSI na SI UGONJWA. Naamini utakubalina na mimi kwamba wengi wao wanavitambua virusi vya Corona kama ugonjwa kitu ambacho si sahihi kumbe ugonjwa wenyewe ni homa kali ya mapafu! Na ndio hapo nasema “KUSHOTO NI TEHAMA halafu kulia kuna VIRUSI VYA CORONA“.

INAYOHUSIANA  Youtube kuleta uwezo wa kuwa mubashara kwenye Android

Nini mantiki yake?

Najua wengi wenu mtasema ni namna mojawapo ya kufikisha ujumbe kirahisi kwenda kwa jamii lakini tujiulize Mtanzania huyu akitoka leo akaenda nchi ya jirani na akasema “Ugonjwa wa Corona” badala ya “Virusi vya Corona” ataonekana amekosea ama?. Sisi ambao tunazungumza Kiswahili, tunasikiliza habari kutoka mashirika ya kimataifa mathalani DW Ujerumani, Shirika la Afya Duniani tujiulize tumewahi kusikia wakihabarisha kwa kusema ‘UGONJWA WA CORONA?’.

INAYOHUSIANA  Apps Za Mahusiano Zahusishwa na Ongezeko la Maambukizi ya Magonjwa ya Ngono
Kushoto
Maneno sahihi kwa kumaanisha COVID-19.

Watanzania tusipende kuwa wagumu wa kujifunza na kushika kile kilicho sahihi. Hebu tuwe na tabia ya kufikiria kuwa kuna siku unaweza ukaongea kwenye kadamnasi ukawa kituko au lulu kwa wasikilizaji hapa nikimaanisha “CORONA SI UGONJWA” bali ni VIRUSI VINAVYOSABABISHA HOMA YA MAPAFU.

Dunia haisumbuliwi na ugonjwa wa Corona ila virusi vya Corona na TeknoKona kwenye makala zetu tumekuwa tukihabarisha janga hili kama virusi na katu si ugonjwa!.

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Masuala yanayohusu virusi vya Corona kwenye YouTube
    October 14, 2020 at 10:56 pm

    […] leo hii Dunia bado inahangaishwa na janga la virusi vya Corona ambalo bado limeendelea kughasrimu maisha ya watu siku hadi siku. Kutokana na utandawazi taarifa […]