fbpx
Afya, Nokia

Corona nchini India: Nokia wafunga kiwanda kwa mara ya pili

corona-nchini-india-nokia-wafunga-kiwanda-kwa-mara-ya-pili
Sambaza

Baada ya kukifunga kiwanda chake kimoja kwa muda kutokana na Corona, Nokia waliamua kukifungua tena hivi karibuni kutokana na maambukizi kupungua. Wiki hii wamejikuja wakikifunga tena kiwandao hicho baada ya wafanyakazi wengine 42 kukutwa na maambukizi ya Corona.

Corona nchini India nokia
Moja ya Kiwanda cha Nokia nchini India. Chennai.

 

Kiwanda hicho cha vifaa vya mawasiliano kinachomilikiwa na Nokia kipo kusini mwa jimbo la Tamil Nadu nchini India. Kiwanda kilikuwa kimefungwa kwa muda mrefu kuendana na sera ya serikali ya kusimamisha shughuli za kiuchumi na za kijamii kama njia ya kupambana na Corona.

INAYOHUSIANA  Machache kuhusu Nokia 7.1

Nokia walifungua kiwanda hicho tena hivi karibuni baada ya sheria kulegezwa baada ya kuonekana maambukizi ya Corona yameporomoka katika eneo hili. Kufunguliwa kuliendana na kuendelea kuwapima wafanyakazi mara kwa mara na ndio imeonekana kuna ulazima wa kufunga tena kiwanda hicho kwani bado maambukizi yanatokea kwa wafanyakazi wake.

Janga la Corona limeathiri sana viwanda vinavyohitaji wafanyakazi wengi kwa ajili ya kazi zake. Katika kipindi hicho hicho makampuni yanayotengeneza roboti wanaoweza kusaidia kazi mbalimbali za viwandani wanaendelea kutishia upotevu wa ajira nyingi za watu ata baada ya janga la Corona kuisha.

INAYOHUSIANA  Nokia wapo kwenye kununuliwa kilazima, uongozi wake hautaki
Corona nchini India Oppo
Corona nchini India: Si Nokia tuu ndio wamelazimika kufungua na kufunga kiwanda, Kampuni ya Oppo pia imejikuta ikifanya uamuzi huo

Kwa nchini India si Nokia tuu walioathirika kutokana na Corona, kampuni ya Oppo pia ililazimika kukifunga tena kiwanda chake cha simu kilicho jiji la New Delhi baada ya wafanyakazi tisa kupimwa na kukutwa na Corona baada ya siku chache ya kuanza tena kazi katika kiwanda chake.

Vyanzo: EconomicTimes na tovuti mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |