fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps Kompyuta Teknolojia Windows 11

Windows 11 kuzinduliwa bila ya programu tumishi za Android

Windows 11 kuzinduliwa bila ya programu tumishi za Android

Spread the love

Habari kuhusu Windows 11 zimekuwa ni nyingi katika miezi ya karibu zikiongelea mambo mbalimbali yanayoihusu programu hiyo endeshi na hata hivyo bila ya kuwa na uwezo wa kukubali programu tumishi za Android ndani yake.

Windows 11 ndio toleo linalofuata baada ya Windows 10. Ujio wa Windows 11 haimanishi hii ya sasa itafikia ukingoni hivi karibuni kwa maana ya kwamba kuendelea kupokea masasisho la hasha! Lakini ni vyema tukawa tayari kuboresha kompyuta zetu na kuhamia kwenye toleo linalokuja.

SOMA PIA  Hii ndio Xiaomi Mi 11 Ultra

Moja ya sifa ambayo Windows 11 inayo ni uwezo wa WhatsApp, Instagram. Spotify, n.k kufanya kazi kwenye toleo hilo la programu endeshi. Hilo halijabadilika ila itakapozinduliwa Oktoba 5 mwaka huu haitakuwa na uwezo wa programu tumishi za Android kufanya kazi.

programu tumishi za Android

Programu tumishi mbalimbali za Android kwenye Windows 11.

Je, ni lini zitaanza kufanya kazi?

Kutofanya kazi kwa programu tumishi siku ya uzinduzi wa Windows 11 si kwamba mambo yatakuwa hivyo hivyo tuu daima hapana, bali zitaruhusiwa huko mbeleni kwa ambao tayari watakuwa wanatumia toleo hilo la programu endeshi kikamilifu. Kwa sasa Windows 11 inapatikana kwa baadhi ya watumiaji mbalimbali ambao wanaijaribu kabla ya kuzinduliwa na hatimae kupatikana kwa watu wengine pia.

programu tumishi za Android

Uwezo wa programu tumishi kufanya kazi kwenye WIndows 10/11 kunapunguza utegemezi wa simu janja ili kuperuzi kwenye mitandao hiyo ya kijamii.

Kuna mengi ambayo tutaweza kufahamu Windows 11 kabla ya uzinduzi wake mnamo Oktoba 5. Hivyo, endelea kutufuatilia kila siku na tutazidi kuwahabarisha masuala mbalimbali yanayohusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania