Kwenye dunia ya leo watakuwepo watu wachache ambao hawajui mtandao wa kijamii uitwao Twitter ambapo unawezesha kuchapisha vitu mbalimbali lakini umejitofautisha na mitandao mingine.Mpaka sasa una chapisho lako kwenye Twitter?
Katika njia ya upashaji habari inawezekana kabisa ukawa unatumia Twitter kuweka chapisho lako au kutuma ujumbe kwa watu unaowafuata. Lakini pengine wewe ni mmoja wa watumiaji hai (mara kwa mara) wa mtandao wa kijamii husika. Je, unafurahishwa na mtu yeyote kuweza kujibu kwenye kile ulichokichapisha?
Katika siku za usoni Twitter inatarajia kuwapa uwezo watumiaji wake kuamua nani anaweza akajibu kitu kwenye chapisho aliloliweka? Kwa maana ya kwamba utaweza kuchagua iwapo mtu yeyote aweze kukujibu ama wale wanaokufuata (wafuasi wako) au mtu/watu ambao umewataja kwenye chapisho husika.

Hali ikoje hivi sasa?
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamepata bahati ya kuwa miongoni mwa wale wanaofanyia majaribio kitu hicho basi utakuwa umeshayaona maboresho hayo lakini ikiwe wewe ni kama wengine tuu ambao wanakisubiri kuona mambo mapya fahamu ya kuwa hivi sasa iwapo hujafanya wasifu wako kwenye Twitter (uwe faragha) au akaunti yako haijazuiliwa basi mtu yeyote yule anaweza kujibu kwenye kile ambacho umekichapisha.
Maboresho hayo yanaweza kuwa shubiri kwa wengine kutokana na kwamba wanaweza wasiwe na uhuru wa kusema kile walichonacho akilini mwake akijibu kilichochapishwa na mhusika. Vipi wewe unasubirikipengele hicho kwa bashasha?
Vyanzo: The Verge, Business Insider