fbpx
Tecno, Teknolojia

Simu Janja ‘Phantom 9’ Kutoka TECNO Hii Hapa!

tecno-phantom-9

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Simu janja za Tecno zipo lukuki sokoni na zina wateja wengi sababu rahisi ni kwamba bei yake inahimilika (rahisi). Unakumbuka Tecno Phantom? Sasa ni toleo la kenda (9).

Muonekano Wa Nyuma Na Mbele Wa Phantom 9
Muonekano Wa Nyuma Na Mbele Wa Phantom 9

Wateja wengi wa simu janja wanaweza kuwa kwenye wakati mgumu hasa akiwa ni mpenzi wa rununu za Tecno kutokana na kwamba zipo nyingi sokoni vilevile sifa zake zinavutia. Sisi kama wafuatiliaji wa masuala ya teknolojia tukakutana na habari kwamba toleo la kenda kutoka familia ya Phantom limetoka.

Dhima kuu ya kauli hii ni kuwa hakikishia watumiaji wasimu za TECNO juu ya ubora na uimara zaidi utakaoletwa na kumpuni hii pendwa nchini na kwenye bara kwa ujumla. Kwa sasa, TECNO inashika nafasi ya 5 Afrika kama kampuni ya simu pendwa.

INAYOHUSIANA  Snapchat Waanzisha Ma'Group' Na Vipengele Vingine, Sasa Chat Mpaka Na Watu 16!

Sifa kamili za Phantom 9 ni kama ifuatavyo:-

NETIWEKI Teknolojia GSM / HSPA / LTE
UZINDUZI Tangazo Julai,2019
Rasmi 25 Julai 2019 (Kwa Tanzania)
JUMBA Ukubwa 158.5 x 75.3 x 7.9 mm (6.24 x 2.96 x 0.31 in)
Uzito 164.4 g (5.78 oz)
Laini Laini Mbili (Nano-SIM)
KIOO Mfumo AMOLED capacitive touchscreen, 16M colors
Saizi 6.39 inches, 100.2 cm2 (~84.0% screen-to-body ratio)
Ubora 1080 x 2340 pixels, 19.5:9 ratio (~403 ppi density)
Ulinzi Wa Kioo Corning Gorilla Glass 3
UENDESHAJI OS Android 9.0 (Pie)
Chipset Mediatek MT6765 Helio P35 (12nm)
CPU Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A53 & 4×1.8 GHz Cortex-A53)
GPU PowerVR GE8320
UJAZO Memori Kadi microSD, mpaka TB 1 (unaweza ukaongeza mwenyewe)
Ujazo Wa  Ndani 128 GB, 6 GB RAM
INAYOHUSIANA  Windows 10 Kuuzwa katika USB - Flash Disks
KAMERA KUU Kamera Tatu 16 MP, f/1.8, PDAF
8 MP, f/2.4, 13mm (ultrawide)
2 MP, f/2.8, depth sensor
Sifa Zake LED flash, HDR, panorama
Video 1080p@30fps
KAMERA YA MBELE Moja 32 MP, f/2.0
Sifa Yake HDR
Video 1080p@30fps
SAUTI Loudspeaker Ndio (Ipo)
3.5mm jack Ndio (Ipo)
TEKNOLOJIA MAWASILIANO WLAN Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac, dual-band, Wi-Fi Direct, hotspot
Bluetooth 5.0, A2DP, LE
GPS Ndio, inakuja na A-GPS
Radio FM radio
USB microUSB 2.0, USB On-The-Go
VIPENGELE VINGINE Sensa Fingerprint (tena kwenye kioo), accelerometer, gyro, proximity, compass
BETRI Betri halitoki  Li-Ion 3500 mAh

Nisikuchoshe sana, hakika simu hii imekuja na muundo wa kipekee na mzuri zaidi wa kuvutia. Kilicho nivutia mimi zaidi ni Kamera tatu za nyuma, kamera ya mbele, kioo kikubwa na kizuri zaidi chenye muundo wa “dot notch” kwa juu pale katikati.

INAYOHUSIANA  Bill Gates: Kosa kubwa la muda wote ni kuiacha Android kuongoza

Tumekua tukiona makampu ni mengi ya simu yakiondoa tundu la kuchomeka earphone; lakini hapa kwenye Phantom 9 TECNO wameona watuachie “earphone jack” ambayo ipo upandewa chini wa simu hiyo.

We unaona ni jambo gani limekuvutia sana kutoka toleo hili?Endelea kutufuatilia kwa ajili ya kupata sifa nyingine nyingi pamoja na maelezo ya undani kabisa kuhusiana na TECNO Phantom 9.

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Sehemu Ya Maoni Wewe Umevutiwa Na Kipi, Pia Kumbuka Kutembelea TekoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

 

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com