fbpx

Fahamu maana na kazi ya CC na BCC kwenye barua pepe

0

Sambaza

Watumiaji wengi wa barua pepe (e-mail) wanapoingia kwenye uwanja wa kutuma ujumbe katika akaunti zao ama iwe Gmail, Yahoo, Microsoft Outlook, Live Mail, na Mozilla Thunderbird, kuna sehemu inayoonesha CC na BCC.

Lakini wapo baadhi ambao wamekuwa hawaelewi nini maana ya hizo herufi na nini matumizi yake kuwepo hapo. Leo kupitia tovuti yako ya teknokona tutakufahamisha kwa lugha nyepesi na unayoielewa.

Maana ya CC na BCC

CCing inasimama badala yaCarbon Copying na BCCing inasimama badala ya Blind Carbon Copying. Zote mbili, CC na BCC zinakuwezesha kuwatumia watu wengi kwa wakati mmoja ujumbe au mafaili unayokusudia kuwapelekea.

maana na kazi ya CC na BCC

Kuona na kutumia CC au BCC ni pale unapofungua uwanja wa kutuma barua pepe yako sehemu ya kuandika barua pepe kwa unayemtumia ndipo utapoona hizo CC na BCC.

Yaani unaweza kuwatumia ujumbe kwa njia ya barua pepe watu 20 au zaidi kwa wakati mmoja bila ya kupata taabu ya kumtumia mtu mmoja mmoja; ni kitendo cha kuweka barua pepe zao kwenye kipengelecha BCC/CC na kuwatumia mara moja.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya kujitoa au kutoa namba yako kutoka kwenye app ya TrueCaller (2019)

Pamoja na kufanana kwa kazi ya kuwatumia watu wengi kwa wakati mmoja, lakini kuna tofauti ndogo baina ya CC na BCC:-

Unapotumia njia ya ‘CC’ kuwatumia watu wengi ujumbe, ni kwamba kila mmoja ataweza kuona orodha kamili ya wapokeaji wengine waliotumiwa ujumbe huo; kila aliyetumiwa ataona na barua pepe za wengine waliotumiwa ujumbe kama wake.

Kama utahitaji kuwatumia watu wengi ujumbe wa aina moja na kila mmoja asijue mwingine aliyetumiwa basi matumizi ya ‘BCC’ yatakuhusu. Kupitia kipengele cha BCC kwenye barua pepe utaweza kuwatumia watu wengi lakini kila mmoja ataona ujumbe wake bila ya kujua kama kuna mwingine ametumiwa kama huo.

maana na kazi ya CC na BCC

Matumizi ya BCC au CC kwenye barua pepe ni yanasaidia kwenye faragha (kama hupendi mtu mwingine ajue umetumia ujumbe ulele) au kumshirikisha mtu mwingine kwenye jambo hilo hilo kwa wakati mmoja.

Bila shaka kwa yule ambaye hakuwahi kujua kuhusu CC na BCC kwenye barua pepe atakuwa ameelewa na kuelimisha wengine.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.