fbpx
Maujanja

Je ni sahihi kuacha Chaja kwenye Umeme baada ya Kuitumia? #Maujanja

simu-laptop-kuacha-chaja-kwenye-umeme-baada-ya-kutumia
Sambaza

Kuacha chaja kwenye umeme baada ya kuitumia? Ni jambo ambalo nina uhakika ujawahi lifikilia na kujiuliza; Je kuna athari yeyote? Je chaja itaendelea kutumia umeme? Leo fahamu zaidi 🙂

Kuacha chaja kwenye umeme baada ya kutumia
Kuacha chaja kwenye umeme baada ya kutumia – Wengi huwa tunafanya hili

Je chaja ikiwa bado imebakia imechomekwa huwa inatumia umeme?

> NDIYO!

Ata pale ambapo haujachomeka simu au kompyuta yako bado umeme unakuwa unatumika INGAWA ni kiasi kidogo. (Kumbuka hapa tunamaanisha pia ya kwamba switchi ya umeme ikiwa ipo imewashwa).

Kwa mfano uchunguzi uliofanywa na mtandao wa HowToGeek uligundua ya kwamba kama nyumba ina chaja sita na zote zikawa zimeachwa kwenye umeme basi kwa mwaka mzima kuna uwezekano kiasi cha umeme cha takribani kilowatt (kWh) 2.628 zitakuwa zimetumika.

INAYOHUSIANA  WhatsApp ya giza kwenye Chrome, Safari, FireFox

Wakati pia utafiti uliofanywa na mwandishi mmoja wa mtandao wa ZDNet ulitambua ya kwamba kwa chaja moja ya simu ya iPhone ikiachwa kwenye umeme kwa kipindi cha mwaka mmoja itakuwa imetumia kiasi cha kWh 1.5.

Kwa kifupi haijalishi, kikubwa zaidi ni kutambua ya kwamba chaja zitaendelea kunyonya umeme kiasi flani pale zinapoachwa kwenye umeme.

Inasemekana pia kwa chaja feki na za chini ya kiwango basi ndio zitatumia umeme mwingi zaidi.

Inakuwaje chaja iendelee kutumia umeme ata pale ambapo simu au kompyuta haijachomekwa?

Chaja zote zina ka’transfoma kadogo ndani yake. Haka ndio kanakuwa bado kameunganisha mfumo wa umeme.

INAYOHUSIANA  Apple wafanya iwe vigumu zaidi ku'hack iPhone kwa Kuzima Uwezo wa USB

Je kuna umuhimu wowote wa kuhakikisha tunazima au kuchomoa chaja zetu baada ya kutumia?

> Ndiyo!

Inasemekana kwa nyumba yenye chaja kadhaa basi uamuzi wa kuzima umeme au kuchomoa chaja baada ya kutumia zinaweza kuwahikikishia wanaokoa kiasi flani cha pesa kila mwaka.

Pia kuacha chaja hizi zikiendelea kupata umeme kwa muda mrefu ata pale ambapo hatuzitumii tunazifanywa ziwahi kuchoka ndani yake na hivyo kuwahi kuharibika ukilinganisha na kama tungekuwa tunazitumia kiusahihi.

INAYOHUSIANA  Mbinu Ambazo Huenda Huzijui Katika Google PlayStore!

> Pia kuna hatari ya milipuko/shoti ya umeme!!!!

Hili ni hasa kwa pale chaja za chini ya ubora – chaja feki, zinapotumika. Chaja za namna hii kuwepo kwenye umeme kwa muda mrefu kuna weza sababisha shoti na hivyo kukuweka wewe na mali zako hatarini.

umeme kuacha chaja kwenye sokoti
Soketi iliyoungua kutokana na mtu kuacha chaja kwa muda mrefu bila kuzima

Ni kitu kidogo tuu, zima switchi ya umeme baada ya kutumia chaja yako, kama bado hili ni jambo kubwa basi chomoa tuu. Endelea kujifunza mengi kupitia TeknoKona! Kumbuka ku’share na marafiki!

Vyanzo: HowToGeek, ZDNet na mingine mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |