Kampuni ya Transsion Holdings ambayo ndio wazalishaji wa simu za Tecno Apr 5 walizindua simu janja mpya ya Tecno Camon X katika tukio lililofanyika jijini Lagos, Nigeria.
Sambamba na Tecno Camon X pia simu zingine zilizozinduliwa siku hiyo ni Tecno Camon X Pro, Tecno F1, Tecno F2 na Tecno POP1. Tecno Camon X na X Pro zinatofauti katika diski uhifadhi na RAM vingine vyote vinafanana.
Maelezo ya kina yakitolewa wakati wa uzinduzi wa simu rununua Tecno Camon X na nyingine kadhaa.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri wa Mawasiliano wa Nigeria, Bw. Abdur-Raheem Adebayo Shittu ambaye aliishukuru kampuni ya Transsion Holding kwa kutoa ajira 3,000 kwa Wanaigeria na aliwaambia ni muhimu kwa kampuni hiyo kuwekeza zaidi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Mapema katika mkutano na waandishi wa habari Meneja mkuu wa Transsion Holdings, Bw. Stephen Ha alisema Camon X inakuja na kipengele cha picha bora na hakika kwa wapenzi wa Selfie itawafurahisha sana.
Aidha, Tecno walitangaza kuingia ushirika na kampuni ya Google ili kuimarisha uzalishaji wa simu nyingi zitakazokuwa na bei nafuu kwa watumiaji wengi barani Afrika.
Uzinduzi wa Tecno Camon X Pro ambao uliwajumuisha watu mbalimbali siku hiyo.
Sifa za TECNO Camon X
Aina ya kioo: IPS LCD Ukubwa wa kioo: 6 inchi (18:9)
Mfumo endeshi: Android 8.1 Oreo Aina ya Prosesa: MediaTek Helio P23 Ukubwa Prosesa: Octa-core 2.0GHz
Ukubwa wa RAM: 3GB (4GB kwa toleo la Pro ) Uhifadhi wa ndani: 16GB (64GB kwa toleo la Pro) Memori kadi ya nje: Ukubwa mpaka 128GB
Teknoloji mawasiliano: 4G LTE SIM: Laini mbili
Kamera ya nyuma: 16 MP, Ring flash Kamera ya mbele: 24 MP, dual-flash
Ukubwa Betri: 3750mAh Aina ya Betri: Li-Po Rangi ya simu: Midnight Black Ulinzi: Fingerprint (rear-mounted), Face ID
Selfie katika simu hii itatoa picha zenye ubora hata kushinda zile za kamera ya nyuma kama ilivyozoeleka kwa simu nyingi. Tecno Camon X inakuja na kamera ya mbele (Selfie) yenye megapixel 24 na kamera ya nyuma ikiwa na megapixel 16.
Mbali na Tecno Camon X pia Tecno ilitangaza uzinduzi wa simu zake za familia ya F ambazo ni Tecno F1, Tecno F2 na Tecno POP1 (a.k.a Tecno F3). Simu hizi zote zitakuwa na mfumo endeshi wa Android Oreo (Go edition).
Karibu zote zinafanana sifa zake kuu na tofauti ni kwenye kamera ambapo Tecno POP1 itakuwa na kamera ya mbele yenye megapixel 5 na ya nyuma megapixel 8.
Sifa za Tecno F1, F2 na Tecno POP1
Mfumo endeshi: Android Oreo (Go edition)
Ukubwa wa kioo: inchi 5.7, 18:9 Kamera ya nyuma: 8MP Kamera ya mbele: 2MP selfie camera (5MP kwa POP1) Prosesa: 1.3GHz quad-core MT6735 Ukubwa Betri: 3000mAh Ukubwa wa RAM: 1GB RAM Uhifadhi wa ndani: 16GB Ulinzi: Fingerprint sensor
Simu ya Tecno F1 ni ya uwezo wa kawaida ambao imelenga zaidi watu ambao wana matumizi ya kawaida sana lakini wanatumia simu janja.
Simu zote bei yake bado haijawekwa wazi lakini ndani ya mwezi huu zitaanza kuuzwa. Umefurahishwa na simu rununu mpya kutoka Tecno?
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.