fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu TCL Teknolojia

Tufahamu ya muhimu kuhusu simu janja TCL L10 Pro

Tufahamu ya muhimu kuhusu simu janja TCL L10 Pro

Spread the love

TCL kampuni ambayo wengi wanaifahamu kwa bidhaa za runinga janja lakini hata upande huu wa rununu wapo na wamekuwa wakitoa simu hizi za kisasa hivyo kuwafanya kuwa washindani. Mwezi huu wa Septemba wameamua kutoa simu janja TCL L10 Pro.

Septemba hii imeonekana kwamba isipite hivi hivi tuu bila ya TCL kutoa simu janja ya kwao ambayo kimsingi haina mengi; kwa lugha rahisi ni rununu ambayo inafaa kwa matumizi ya kawaida ambayo inafanya mtumiaji kuperuzi vizuri tuu mtandaoni pamoja na kutumia programu tumishi mbalimbali. Simu hii imezinduliwa huko Brazil na sifa zake ni hizi:

SOMA PIA  Madhara ya kulala na Simu yako ikiwa Imewashwa

Kioo/Muonekano

Hapa unakutana na simu janja yenye kioo cha urefu wa inchi 6.22 aina ya LCD ambacho kina ung’avu wa hali ya juu (unaovutia) huku mwonekana wake wa mbele ukipendezeshwa na kamera ya mbele yenye MP 5, iliyoingia ndani kidogo mithili ya bonde.

Kamera/Memori

TCL L10 Pro ina kamera tatu nyuma ambazo zina MP 13, 5 na 2 halikdhalika zikiwa na taa ya kuongeza mwanga sehemu hafifu. Vilevile, RAM yake ni GB 4 kwa 128GB za diski uhifadhi.

TCL

TCL L10 Pro ina teknolojia ya kutumia alama ya kidle iliyowekwa upande wa nyuma wa simu.

Betri/Mengineyo

Betri ya kwenye simu hii ina uwezo wa 4000mAh, inatumia kadi mbili za simu, kipuri mama cha rununu husika ni Unisoc SC9863A, kasi ya intaneti inaenda mpaka 4G LTE, inakuja na Android 10, WiFi, Bluetooth 4.2 vipo.

TCL

Simu hii ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni na inapatikana katika rangi moja tu-Nyeusi.

Bei ya rununu inakaribia $250|zaidi ya Tsh. 575,000 ukiinunua huko Brazil. Sasa kazi kwako ewe msomaji wetu kufanya maamuzi kwani tayari umeshafahamu sifa za simu janja husika. Kumbuka kuendelea kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii.

Vyanzo: GSMArena, Yuga Tech

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania