fbpx
BIKO, Michezo ya kubashiri, Mitandao ya Simu, Tanzania

BIKO na Vodacom Tanzania wakubalina kufanya biashara zaidi

biko-na-vodacom-tanzania-wakubalina-kufanya-biashara-zaidi
Sambaza

Kwa miaka kadhaa sasa nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wanashiriki kwenye michezo ya kubashiri na anayebahatika anajishindia zawadi mbalimbali. Michezo hiyo imeongeza ukaribu baina ya makampuni husika hivyo basi kutanua wigo wa biashara.

Kila leo wapo washindi wanaojishindia fedha taslimu, pikipiki, n.k jambo ambalo linabadilisha maisha ya mtu kutoka hatua moja hadi nyingine. Lakini hapo hapo hatuwezi kusahau mitandao ya simu ambapo mchakato wote wa kufanikisha unafanyika kwa njia ya simu; kwa lugha rahisi malipo yanaweza kufanyika kwa Tigo Pesa, HaloPesa, M-Pesa au Airtel Money.

Sasa BIKO na Vodacom Tanzania wameingia makubaliano ambapo kwa mteja yeyote ambae atabasiri kwa mwamvuli wa Biko na kulipia kwa njia ya M-Pesa atakuwa na nafasi tatu (3) kwa maana ya kwamba ushindi wa papo kwa papo, kuingia kwenye droo kubwa (Jackpot) na nyingine ni “Biko & M-Pesa”.

Baada ya kupatikana washindi wa kawaida ambao huwa wanatafutwa badada ya hapo itachezeshwa droo maalum kutafuta washindi waliocheza BIKO kupitia M-Pesa na mshindi atapatikana.

BIKO na Vodacom Tanzania
BIKO na Vodacom Tanzania watanua wigo kwa wateja wa M-Pesa kuweza kujiongezea nafasi ya kuibuka mshindi/washindi.

Biashara ni ubunifu na kwa namna moja su nyingine Voda wametafuta namna ya kujiongezea wateja sijui wewe msomaji wetu una mawazo gani. Usisite kutuandikia maoni yako hapo  chini na daima usiache kutufuatilia.

Vyanzo: TBC 1 na Michuzi Blog

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Mkurugenzi wa Vodacom Kushikiliwa na Polisi: Inahusisha Teknolojia & Mapato
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|