fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Facebook Intaneti Teknolojia

Facebook Kuanza Kutumia HTML5 Kucheza Video

Facebook Kuanza Kutumia HTML5 Kucheza Video

Spread the love

Facebook wametangaza kuanza  kutumia HTML5 kucheza video zake katika mtandao kwa vivinjari vyote, hii inamaana kwamba sasa hautahitaji kuwa na plugin maalumu ili kucheza video katika mtandao huo maarufu.

Sababu kubwa kwa mtandao huu kufanya hivyo ni pamoja na kupitwa na wakati kwa plugin maarufu kama flash play.

Kipindi cha nyuma ulikua ukicheza video Facebook basi ilikua inachezeshwa kwa msaada wa kifaa kinaitwa plug in, plug in inatengenezwa na kampuni nyingine (zipo nyingi tofauti tofauti) na sio Facebook. Baada ya kuhudumu kwa muda mrefu plug in zimekuwa na mapungufu mengi hasa ya kiusalama na mitandao kama Facebook imelazimika kuhama aina hiyo ya kuchezesha video ili kuboresha huduma zake.

HTML5

Alama ya HTML 5

Facebook wanafikia hatua hii ili kuwavutia watumiaji wake wa mtandaoni kwa kuwapa huduma bora zaidi, katika kutimiza hilo wanataka kuhakikisha kuwa wao ndio chaguo la kwanza kwa watumiaji linapokuja swala la kuangalia na kusambaza video. Mitandao maarufu mingine kama YouTube pia wamekwisha anza kutumia huduma hii ya kucheza video kwa kutumia HTML5.

SOMA PIA  Kuwa Makini 'Emoji' Moja Inaweza Kutofautiana Kati Ya Simu Na Simu!

HTML  ni sheria zinazotawala utengenezaji wa kurasa za mitandao, kwa lugha nyepesi hizi ni sheria ambazo lazima zifuatwe na yeyote yule anayetaka kuweka kitu katika mtandao. Mpaka sasa kuna matoleo matano ya sheria hizi na kabla ya hili toleo la tano sheria hizi zilikua hazifafanui juu ya kucheza video hivyo kama unataka ukurasa wako kucheza video ulihitaji kutumia plug in.

SOMA PIA  WhatsApp watanua wigo kuhusu uwezo wa kutafuta kitu

HTML5

Kikaragosi cha HTML5

Je wewe umegundua tofauti ya video zinazochezwa na plug in na zile zinazochezwa na HTML5? tushirikishe mawazo na maoni yako juu ya hili.

Endelea kutufuata katika mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania