Mkurugenzi mkuu wa Google Sundar Pichai akijibu maswali katika chuo kikuu cha Delhi amesema kwamba Google inafikiria kuwaruhusu watumiaji wake kupiga kura kuchagua jina la Android 7.0 . Google imekuwa ikitoa majina kwa matoleo yote ya Android na majina haya yanatokana na peremende na vyakula vingine vya utamu (pamoja na ‘ice cream’).
Google wana kamati ambayo inashughurika na utoaji wa majina kwaajiri ya matoleo ya Android, kamati hii hutoa majina ambayo yako katika mtiliriko wa alfabeti, baadhi ya majina ya matoleo yaliyotangulia ni Cupcake, Donut, Eclair, Froyo, Gingerbread, Honeycomb, Ice cream Sandwich, Jelly bean, Kitkat, Lollipop na Marshmallow ambayo ndiyo ya mwisho.
Kama hili litatimia basi huenda kwa mara ya kwanza Android itapata jina la kigeni na na tofauti na majina yaliyotangulia, kwa upande mwingine wataalamu wa mambo wanafikiria hii itakuwa ni moja ya nafasi ya Google kuipa kiki bidhaa yake hiyo inayo shindana na bidhaa za Apple.
Tayari baadhi ya mitandao iliishaanza kukisia jina la Android N ambayo itatoka mwakani, moja ya majina ambayo yalikuwa yanategemewa kutumiwa na Google ni pamoja na Android Nutella, Android Nut, Android Nerds, Android Nutrageous,na Android Nougat.
Je unadhani ulimwengu wa Kiswahili tunaweza na sisi tukaweka mkazo mpaka Google wakaita toleo lijalo la Android jina la Kiswahili ambacho kinaongelewa na watu karibu 150 milioni?
Tuambie katika maoni hapo chini wewe ungeliitaje toleo lijalo la Android kwa kiswahili?
No Comment! Be the first one.