fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti YouTube

Video Maarufu Zaidi Youtube 2015

Video Maarufu Zaidi Youtube 2015

Spread the love

Ni Disemba na hiki ndio kipindi ambacho kumi bora za mwaka huwa hazikauki kila kitengo, leo nitakuletea video maarufu zaidi katika tovuti maarufu ya YouTube kwa mwaka 2015.

Video hizi kumi maarufu zaidi zimeamuliwa na YouTube wenyewe kutokana na marangapi video imeangaliwa, ilipokelewaje? na ilisambaaje.

YouTube huwa wanataja video hizo marufu katika chaneli yao inayokwenda kwa jina la YouTube Rewind.Video hizi za maarufu za mwaka 2015 zimegawanywa katika makundi mawili, moja ni ya video za muziki na kundi la pili ni video za kawaida kama matangazo ucheshi na vipindi vya television.

youtube-rewind-2015

Picha ya jarada la video maarufu za mwaka 2015

Video maarufu zaidi za upande wa muziki.

1.Wiz Khalifa – See you again

Wimbo huu uliotumika katika filamu maarufu ya Fast Furious 7 ya mwaka 2015, na ulipendwa zaidi kwa kuwa uliimbwa kama kumbukumbu ya Paul walker mmoja wa wacheza filamu hiyo aliyefariki dunia mwaka 2013 wakati filamu hii ikitengenezwa.

SOMA PIA  Vitu vinavyofanyika kwenye intaneti ndani ya dakika moja #2019

Video ya wimbo huu imeangaliwa zaidi ya  mara bilion moja.

2. Maroon 5 – Sugar.

Hii ni video maarufu namba mbili kwa mwaka huu wa 2015 na mpaka sasa imekwisha tazamwa karibu mara milion miatisa ishirini. Sugar ni wimbo ulio katika album ya tano ya studio ya bendi hiyo kutoka nchini Marekani, hii albamu ilirekodiwa mwaka 2014 na video ili chapishwa mwezi Januari.

3. Ellie Goulding – Love me like you do.

Huu ni wimbo unaotoka katika ablamu ya DELIRIUM ya msanii Ellie, video hii ilichapishwa mwezi January mwishoni na mpaka sasa imekwisha tazamwa zaidi ya mara milioni mia nane na hamsini.

4. Major Lazer & DJ snake – Lean On

Hii ni video ilichapishwa YouTube mwezi wa tatu mwishoni na ikaweza kujipatia umaarufu kwa kasi, mpaka sasa imekwisha tazamwa zaidi ya mara milioni mia tisa.

SOMA PIA  Japani watakuwa vizuri kwenye huduma ya intaneti ya 5G kufikia 2020

5. Taylor Swift – Bad blood

Katika nafasi ya tano anasimama Taylor Swift na video ya wimbo wake Bad blood ambao umetazamwa zaidi ya mara milioni mia sita tangu ilipochapishwa hapo mwezi Mei.

6. David Guetta – Hey Mama

Hey Mama ni video maarufu namba sita ambayo tangu ilipochapishwa imeweza kutazamwa zaidi ya mara milioni miatano, video ya wimbo huuu imechapichwa YouTube mwezi Mei

7. Sia – Elastic heart

Ingawa video hii ilipigiwa kelele na watetea haki za watoto baada ya kumuonesha mtoto akipigana ndani ya banda lakini hilo halikuizuia kuweza kuangaliwa zaidi ya mara milioni mia nne sabini tokea ilipochapishwa mwezi wa Januari.

8. Fifth Harmony – worth it

SOMA PIA  Sheria ya makosa ya Kimtandao: Jamii Media yaipinga.

Hii ni video kutoka kwa kundi ambalo lilitokana na kipindi cha runinga cha kutafuta vipaji cha X factor, wakimshirikisha  msanii kid ink wameweza kutazamwa zaidi ya mara milioni mia nne tisini. Ingawa video yao imetazamwa zaidi na mtandaoni kushinda video iliyopo namba saba  hii ni kwa sababu kigezo sio tuu marangapi video imetazamwa mtandaoni.

9. Adele – Hello

Ikiwa haina wiki nyingi tangu iwekwe mtandaoni mwezi Oktoba video hii ya mwanadada Adele imekwisha tazamwa zaidi ya mara milionI mia Saba. Huu ni wimbo kutoka katika albamu mpya ya adele inaitwa 25.

10. Silento – Watch me

Wengi wanaujua huu wimbo kama whip Nae Nae, ni wimbo uliojipatia umaarufu hasa kwa staili za uchezaji zinazoonyeshwa na wahusika. tangu kuchapishwa imekwisha tazamwa zaidi ya mara milioni mia nne themanini.

Je ni video gani ya mwaka huu iliyopo YouTube ungefurahi kama ingeingia kwenye orodha hii?

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania